TEA YAWAFADHILI MAFUNZO AKINA MAMA NA VIJANA ZAIDI YA 4,000


 Mkurugenzi wa Miradi na Utafutaji Rasilimali kutoka TEA,Waziri Salum akiongea na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Ubunifu jijini Dodoma 2022.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Philip Mangula akifafanua jambo kwa wanahabari baada ya kutembelea banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kupata taarifa kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akifafanua jambo kwa wanahabari kuhusu miradi inayosimamiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) alipotembelea banda la TEA katika maonyesho ya MAKISATU 2022.

Wananchi mbalimbali wakipata elimu na huduma katika banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania  kwenye maonyesho ya MAKISATU 2022..

Na Asha Nwakyonde,Dodoma

MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA), imewapatia ufadhili wa mafunzo akina mama na vijana zaidi ya 4000 nchi nzima kwa lengo la kukuza bunifu mbalimbali na  ujuzi wa kujiari wenyewe ili waweze kukabiliana na changamoto za ajira.

Akizungumza Mei 18, 2022 katika maonyesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia( MAKISATU), kwa mwaka 2022 ambayo yameendaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP),kupitia mradi wake wa FUNGUO, yanayofanyika katika viwanja vya Jamuhuri jijini hapa.

Mkurugenzi wa Mradi na Utafutaji Raailimali kutoka TEA, Waziri Salumu amesema lengo la kushiriki maonyesho hayo ni kwa ajili ya kipengele cha ubunifu na kukuza ujuzi .

Amesema kuwa wameshiriki maonyesho hayo kwa kuwa wao ni wadau wakubwa ambayo yapo chini ya wizara ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwanadi wabunifu wao.

Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa ufadhili wanatoa kwa akina mama na vijana ili waweze kujiari wenyewe.

"Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), ni taasisi ya serikali ambayo ipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tumekuja hapa kwenye mabanda kwa ajili ya kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na TEA," amesema.

Amesema kuwa moja kazi za mamlaka hiyo ni kusimamia Mfuko wa Taifa wa Elimu katika mfuko huo mamlaka hiyo inashughulika  zaidi kuboresha na kujenga miundombinu ya elimu kama vile madarasa, nyumba za walimu, mabweni na mabwalo.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa TEA ina majukumu ya kusimamia mfuko wa kukuza ujuzi kwa wabunifu mbalimbali na kwamba wapo vijana wanaotengeneza simu za kiganjani, akina mama wanasindika mvinyo kupitia uyoga.

" Pia tuna vijana tunawapa mafunzo ya kusindika asali lakini kuna kijana mwingine tumempa mafunzo ya namna gani ya kutengeneza mashine  bayogesi 'biogesi' na baadae kupata mbolea ya  asili 'Oganic' amesema Mkurugenzi huyo.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanafadhiliwa na mamlaka ya elimu ya Tanzania kupitia serikali.

Kwa upande  wake Meneja wa miradi ya elimu pia ni Mratibu wa mfuko wa kuendeleza ujuzi kutoka TEA, Masozi Nyerenda amesema kuwa mamlaka hiyo inasimamia mifuko miwili mfuko wa  kuendeleza ujuzi ( SDF),na ubunifu.

"Tupo hapa kwenye maonyesho haya ya ubunifu  kwa ajili ya kuwaonyesha wananchi, Watanzania kuhusiana na miradi ambayo tunaifadhili kwa upande wa mfuko wa elimu na ule wa kuendeleza ujuzi," amesema  Meneja huyo.










Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA