Mbunifu kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT),Joel Ngushwai akielezea namna ya kifaa cha cha kubebea watoto waliozaliwa njiti kinachoitwa Upendo Blanketi katika Maonyesho ya Wiki ya ubunifu 2022.
Na Asha Mwakyonde,Dodoma
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),imetengeneza vifaa vya kumsafirishia mtoto aliyezaliwa njiti kutoka wodi moja kwenda nyingine (Transport Incubator) na Upendo Blanketi kutokana na changamoto za usafirishaji watoto hao.
Akizungumza Mei 18,2022 katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia (MAKISATU),kwa mwaka 2022 ambayo yamaeandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa kimataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP),kupitia mradi wake wa FUNGUO, yanayofanyika katika viwanja vya Jamuhuri jijini hapa, Mbunifu kutoka DIT Joel Ngushwai amesema kuwa utafiti walioufanya katika Hospitali mbili za Amana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),waligundua kuna changamoto vifaa hivyo.
Mbunifu huyo amesema kuwa changamoto iliyopo ni usafirishaji wa mtoto kutoka wodi moja hadi nyingine na kwamba watoto hao wanashida ya joto hawawezi kuzalisha joto katika miili yao hivyo wanategemea kutoka nje.
Ameongeza kuwa katika utafiti wao waliofanya hospitali hizo wamebaina wodi za kujifungulia akina mama, na vyumba vya Uangalizi Maalumu ( ICU),zipo mbali kama mita 100 hadi 200 anapotakiwa mtoto kulazwa kutoka na umbali huo inaweza kumsababishi mtoto huyo kupoteza maisha au kupata matatizo mengine kwa kushindwa kuzalisha joto lake la mwili.
"Tumekuja na vifaa hivi ambavyo ni transport Incubator na Upendo Blanketi vinaweza kumsafirisha mtoto salama kutoka wodi moja kwenda nyingine au hospitali moja kwenda nyingine" amesema mbunifu huyo.
Amefafanua kuhusu kifaa cha upendo blanketi kimeongezwa sehemu ya kumuongezea mtoto joto ambayo itawekwa chupa ya maji ya moto na mtoto atasafirishwa kutoka wodi moja hadi nyingi au hospitali moja hadi nyingine bila kupata tatizo lolote," amesema.
Mbunifu huyo Ngushwai ameeleza kuwa malighafi zilizotumika kutengeneza kifaa hicho ni laini na kwamba mtoto hawezi kuumia lakini pia kifaa hicho kimetengenezwa na zipu hata ikitokea bahati mbaya mtu amejikwaa mtoto huyo hawezi kudhurika endapo ataanguka.
MAJARIBIO
Mbunifu huyo amefafanua kuwa tayari kifaa hicho walishakipeleka katika hospitali ya Amana kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ambapo kimeonekana kufanya kazi vizuri.
" Kwa sasa tunajiandaa kushirikiana na Kampuni Tanzu ya DIT kwa ajili ya kufanya utafiti na kwa siku kupitia Design Studio tunaweza kuzalisha zaidi ya kumi," amesema, " mbunifu huyo.
Amesema kuwa kifa cha Transport Incubator matumizi yake hayatofautiani na Upendo blanketi kazi yake ni ile ile isipokuwa inatumia umeme kuonyesha hali halisi ya mtoto inavvyoendelea.
"Tulikwenda Mkoa wenye baridi kuona ni kwa namna gani inavyoweza kufanya kazi tulienda Mkoa wa Songwe tukafanya majatibio na madaktari walisema kinafanya kazi vizuri na walitamani tuwatengeneze lakini bado tunasubiri zipitishwe na mammlaka husika kama Wizara ya afya," amesema.
GHARAMA
Amesema kuwa kifaa cha Upendo blanketi hadi kufika sokoni kinauzwa laki moja kutokana na upatikanaji wa malighafi zake.
"Na hii ya Transport Incubator inauzawa 400,000 hadi 500,000 kwani malighafi zote zinapatikana hapa nchini hivyo ni rahisi na ikinunuliwa kutoka nje bei yake ni zaidi ya milioni 1.5," amesema.
WITO
Ameiomba serikali irahisishe upitishwaji wa vifaa tiba ili kupunguza utegemezi wa teknolojia kutoka nje pia itasaidia kupunguza vifo vya watoto na akina mama wakati wa kujifungua.
Pia ametoa wito kwa wabunifu wengine kuangalia matatizo yanayowazunguka watu wote katika jamii wasiangalie upande mmoja.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano kutoka Kampuni Tanzu ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT co Ltd), Regina Kumba amesema wao kama taasi bunifu hizo haziishii chuoni na badala yake kupitia kampuni hiyo bunifu zote zinachukuliwa zina boreshwa na kuingizwa sokoni.
Ameongeza kuwa baada ya maonyesho hayo vifaa hivyo vitatafutiwa masoko pamoja na bidhaa nyingine ili ziende zikatatue changamoto katika jamii.
0 Comments