NECTA YAJA NA MFUMO WA UTATUZI WA UFUNDISHAJI

Afisa Mitihani Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Utafiti na Tathimini ya Mitihani kutoka NECTA ,Dk. Alfredy Mdima, akifafanua namna mfumo wa kutatua tatizo la ufundishaji na upimaji wa wanafunzi waliowengi darasani unavyofanya kazi.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

BARAZA la Mitihani Tanzania(NECTA), limebuni mfumo wa kutatua tatizo la ufundishaji na upimaji wa wanafunzi walio wengi darasani  kupita kiasi kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Matifa la kuhudumia Watoto Duniani ( UNICEF).

Akizungumza Mei 18,2022 katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu  wa Sayansi na Teknolojia (MAKISATU),kwa mwaka 2022 ambayo yamaeandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa kimataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP),kupitia mradi wake wa FUNGUO, yanayofanyika katika viwanja vya Jamuhuri jijini hapa, Afisa Mitihani Mkuu wa Kitengo cha Mipango, Utafiti na Tathimini ya Mitihani kutoka NECTA ,Dk. Alfredy Mdima, amesema kuwa mfumo huo ni suluhisho la tatizo la ufundishaji na upimaji wa watoto wawapo darasani.

 Ameongeza kwa sasa kupitia mfumo huo sio tatizo kuwa na wanafunzi wengi darasani kwa kutumia Kishikwambi au simu janja wamechukua mada zote na kuziweka katika simu hiyo pamoja na kuweka maswali ya aina zote ili yaweze kumsaidia mtoto.

Dk.Mdima ameeleza kuwa mfumo huo kwa kiingereza unaitwa Activity teaching model  na kwamba wanafunzi wanapenda kutumia simu hizo kupitia Kishikwamba watafurahia kwa kuwa wanapenda na watajibu maswali na akipata maswali yote  matano atapewa zawadi ya katuni.

" Tumekuja hapa katika maonyesho haya tumeleta mifumo miwili wa kwanza ni mfumo wa kidigitali wa  usaishaji wa mitihani msaishaji anapelekewa mitihani kidigitali na anasaisha kidigitali na anarudisha Necta kwa mratibu wa mitihani kidigitali," amesema.

Amesema kuwa mfumo huo unamrahisishia mwalimu kwa kuwamudu wanafunzi kwani kupitia simu hizo mwalimu huyo atakuwa anamuona mwanafunzi ambaye yupo kwenye mfumo anajibu maswali yake.

"Mfumo huu hauhitaji mtandao  bali watatumia 'bluetooth' ambapo mwalimu na wanafunzi watatumia kwa wakati mmoja.Tumekuja na suluhisho hili tunaomba serikali ituunge mkono" amesema.

Ameeleza kwamba wamefanya majaribio katika wilaya tano ambazo ni Bagamoyo, Mbeya Mjini, Tunduma,Halamashuri ya wilaya ya Mafinga na Wilaya ya Makete wamejiridhisha kuwa mfumo huo unafanya kazi vizuri.

Post a Comment

1 Comments

  1. Ubunifu bora kabisa wa kizalendo. Kazi iendelee . Mifumo ya kieletroniki ndio model bora zaidi kutoka kutatatu changamoto mbali mbali zinazoikumba jamii yetu. HONGERA NECTA

    ReplyDelete

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA