Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman,akizungumza wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
NA IMMACULATE RUZIKA,DODOMA
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema kuwa kazi ya vyuo vikuu ni kufanya tafiti na kuimarisha kwenye ugubduzi na ubunifu wa teknolojia hapa nchini ambazo inawasaidia wabunifu kunufaika na kazi zao.
Pia ametoa wito kwa Wizara ya Elimu, Sanyansi na Teknolojia kwa kushirikiana na taasisi zake Tanzania Bara na Zanzibar kuandaa mikakati Maalamu kwa lengo la kulindi haki za wabunifu.
Makamu Othman ameyasema hayo jana wakati akifungua maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Amesema ubunifu ni nyenzo nzuri na ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya haraka katika sekta ya elimu na katika huduma za jamii endapo itatumika vizuri katika uzalishaji.
Amesema kuwa serikali zote mbili zimeazimia kujenga uwezo wa ndani kuendelea kuweza kwenye rasilimali watu, miundombinu,vifaa vya kisasa vya utafiti,Ubunifu ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano katika taasisi za Sanyansi na Teknolojia.
Makamu Othman ameeleza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wiki hii na ndio maana maonesho haya yanafanyika ili kuendelea kuibua na kukuza vipaji tunapaswa kufanya maonesho naamini itatusaidia kuongeza kasi ya maendeleo kwa taifa.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha na kitaalamu Tume ya Sanyansi na Teknolojia( COSTECH). ili iweze kusaidia zaidi shughuli za utafiti na ubunifu nchini kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Pia Makamu wa Rais amepata fursa ya kutembelea na kujionea bunifu mbalimbali zilizopo katika mashindano hayo na kuvutiwa na bunifu hizo.
Aidha Makamu huyo ameishukuru Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuandaa Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa kwa mwaka huu wa 2022 huku ikiwa na kauli mbiu isemayo “Ubunifu kwa maendeleo endelevu”.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa.Adolf Mkenda,amesema kuwa Taasisi tofauti tofauti 50 pamoja na wabunifu 26 ambao bunifu zao zimefikia hatua ya kuingia sokoni na kuanza kutumika zimeshiriki katika maeonesho hayo.
Amesema kuwa wabunifu 862 walijisajili kwa mwaka huu na wabunifu 86 bunifu zao zitashindanishwa ili kupata washindi.”amesema Prof.Mkenda.
0 Comments