PROF. MKENDA: SERIKALI INATENGA FEDHA ZA KUSOMESHA WAGUNDUZI NJE MIMI NI NANI NIPINGE?

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf  Mkenda  akizungumza  wakati akifungua mdahalo wa  siku mbili wa wadau juu ya ubunifu katika sekta ya umma kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu Makisatu  iliyoanza jana ambayo yanafanyika uwanja wa Jamuhuri  jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia akifafanua jambo   wakati  mdahalo wa  siku mbili wa wadau juu ya ubunifu katika sekta ya umma kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu Makisatu  iliyoanza jana ambayo yanafanyika uwanja wa Jamuhuri  jijini Dodoma.


Baadhi ya wadau wa ubunifu na wa sekta ya Umma wakifuatilia mdahalo juu ya masula ya ubunifu.

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM),imefafanua kuwa serikali  itapeleka Watanzania kwenye vyuo mahiri zaidi duniani kusomea Sayansi, Teknolojia na Tiba.

Pia amesema kuwa serikali itaendelea kuwajali  wabunufu,kuwatambua na kuendeleza vipaji vyao hivyo ina jukumuku la kuwajengea mazingira yatakayochochea ubunifu ili kuongeza idadi yao.

Prof. Mkenda ameyasema hayo  Jijini hapa wakati akizungumza akifungua mdahalo wa  siku mbili wa wadau juu ya ubunifu katika sekta ya umma kwenye maonesho ya wiki ya ubunifu Makisatu  iliyoanza jana amesema kuwa nchi zote duniani zilizoendelea kama China na India  ziliwapeleka watu wake kusoma nchi nyingine kuchota taaluma.

" Watu wote wenye uwezo wa ugunduzi,  sayansi  na teknolojia wakajua kuna fursa wakaja kuonyesha kazi wanazozifanya serikali itasaidiana nao kuhakikisha wakawa na bidhaa kutokana na ugunduzi wao," ameeleza Prof. Mkenda.

Kupitia fursa  hiyo wataongeza idadi ya wabunifu hukubakitole mfano ugunduzi uliofanywa na mtoto mwenye umri wa miaka 10 kujua nani ameingia chumbani kwa na ni wangapi walioingia.

"Katika maonyesho haya mtoto huyu wa  mwenye umri wa miaka 10 ambaye amezindua mfumo wa kufundua mtu anayeingia chumbani na wameingia wangapi naye atashiriki, kuna wabunifu wengine wa mitaani ambao hungundua vitu vingi," amesema.

"Serikali inatenga fedha mimi ni nani hata nikapige haya? .Tukimuona Mtanzania anasoma MIT ambayo ni Teknolojia kubwa duniani sisi tutafurahi tutawapeleka India Instute of Technolog waende wakasome huko," ameongeza:

" Kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inaelekeza Serikali ipekeke wabunifu kusomea Sayansi ,Teknolojia na tiba ," amesema Prof .Mkenda.

Amesema kuwa kwa miaka 10, ijayo Tanzania itakuwa imepiga hatua kwenye masuala ya Teknolojia na kwamba wanachagiza ubunifu unaohusika na   masuala ya Kilimo.
 
Waziri huyo amesema kuwa zama za sasa ni za Sayansi na Teknolojia na sekta ya umma inatakiwa kutenda kazi kwa ubunifu ili kuchochea mabadiliko kwenye utendaji Kazi.

Aidha masema  kuwa katika hilo Serikali imesimika mifumo mbalimbali ili kurahisisha utendaji kazi wa kila siku.

Awali Mkurugenzi wa MurugenziI wa Tume ya Taifa ya  Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Amosi Nungu amesema kuwa ni mwaka wa nane kufanya wiki ya ubunifu hapa nchini na uelewa  unazidi kuongezeka.

"Miaka mitano au minne iloyopita kulikuwa na mbunifu kutoka Mkoa wa Songwe aliyebuni helkopta mwaka juzi alikuja katika maonyesho ya Makisatu serikali ilimchukua na kumpeleka Shirika la Nyumbu ,Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), kwenda kujifunza na amekuja na greji inayotembea kwa kuwa Mkoa  mashine tati ndani ya moja ya kukobo,kusanga na kupurura ambayo inawarahisishia wakulima kurudi na unga nyumbani," amesema Nungu. 

Ameongeza kuwa bunifu kama hizo zimeleta ajira kwa vijana wengine pamoja na kuongeza pato la nchi kwani kuna baadhi wanatoa huduma za bidhaa zao nje ya nchi.

Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa ama COSTECH wameamua kufanyamidaalo ambayo inaonekana  Mubashara Mo
 ( live) Ili wabunifu wengi na Watanzania waweze kuona fursa za masuala ya ubunifu Ili waweze kusaidia.


Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA