DK.GWAJIMA AUPIGA MWINGI AJIRA ZA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Malaamu Dk.Dorothy  Gwajima akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/ 2022.

Na Asha Mwakyonde,Dodoma

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Malaamu Dk. Dorothy  Gwajima ametoa rai  kwa wadau wa maendeleo yakiwamo mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa ajira za muda kwa maafisa maendeleo ya jamii hususan ngazi ya kata ambapo kuna upungufu mkubwa  wa maafisa hao.

Dk.Gwajima ametoa rai hiyo jijini Dodoma leo Mei 30,2022 wakati akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2022/ 2023, amesema kuwa lengo ni kuongeza kasi ya utekelezaji wa afua za kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Amesema kuwa wizara hiyo inatoa wito kwa wote wenye taaluma ya maendeleo ya jamii baada ya kustaafu wajitokeze ili kuendelea kutoa mchango wao kwenye jamii  kama ambavyo taaluma nyingine zimekuwa zikifanya.

" Ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maafisa hawa Wizara itaendelea kuwasiliana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kutatua changamoto na upungufu huu katika ngazi ya kata kwa kuwaajiri kwenye mamlaka ya serikali zamitaa kadri bajeti ya serikali itakavyo ruhusu kila mwaka," amesema Dk. Gwajima.

Aidha Dk.Gwajima ametoa wito kwa maafisa maendeleo ya jamii waliopo katika ngazi za mikoa, Halmashauri na kata kushirikiana na wadau wengine na kuendelea kwa kasi zaidi kuelimisha na kushirikisha jamii kuimarika katika dhana nzima ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

" Naishukuru serikali kupitia wizara ya fedha na mipango kwa kutupatia wizara yetu kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya ukarabati wa majengo na miundombinu katika vyuo vya maendeleo ya jamii," ameasma.



Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI