CHUO CHA MIPANGO CHAPATA WANAFUNZI WENGI MAONESHO YA TCU

Makamu  Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso akimpatia  maelezo mteja aliyetembelea katika banda la Chuo hicho katika Maonesho ya vyuo vya Elimu ya Juu jijini Dar es Salaam.


Makamu  Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso akiwaonesha baadhi ya kozi kwenye kipeperushi  wanafunzi waliotembelea katika banda la Chuo hicho katika Maonesho ya vyuo vya Elimu ya Juu jijini Dar es Salaam.

Na Asha Mwakyonde, Dar es Salaam

CHUO Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini chenye makao makuu yake Jijini Dodoma kimesema  kozi zake zote zipo katika muundo wa ajira na  mwanafunzi anaposoma katika chuo hicho anafasi kubwa ya kuajiriwa  endapo  nafasi za ajira zitatangazwa na serikali.

Pia chuo hicho kinamilikiwa na serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na kimeanzishwa kwa sheria Namba 8 ya mwaka 1980 ya Bunge la Tanzania ambayo kimeipa chuo  majukumu matatu ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri elekezi.

Hayo yameyasemwa Julai 22,2022 na Makamu  Mkuu wa Chuo  hicho anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Profesa Provident Dimoso wakati akizungumza kwenye maonesho ya Vyuo vya Elimu ya Juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU)amesema kuwa wanaomaliza katika chuo hicho wengi wanaweza kujiajiri wenyewe na kuajiri wenzao.

"Tuna mifano mingi wanafunzi wetu waliofanya ubunifu wemeweza kutengeneza ajira zao binafisi na kuajiri wenzao kwenye soko la upande wa sekta binafisi. Natumia fursa hii kuwakaribisha waliomaliza kidato cha nne kwa ajili ya kujiunga na chuo hiki ngazi ya cheti na waliomaliza kidato cha sita kujiunga ngazi ya Shahada 'degree' na wale ambao ufaulu wao ni wa principal pass 1 wanaweza kujiunga na diploma," amesema Prof. Dimoso.

Pia Makamu huyo wa chuo amewakaribisha wanafunzi kujiunga na chuo hicho kwani wanaosoma Shahada wanapata fursa ya kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ( HESLB).

Ameongeza kuwa wana idadi ya kubwa ya wanafunzi ambao wanafikia vigezo vya kusomeshwa na Bodi ya mikopo HESLB, na mkwamba katika maonesho hayo mwitikio ni mkubwa wanafunzi wengi wamejisajili.

Prof. Dimoso amefafanua kuwa chuo hicho kina mabweni pamoja na maktaba ambayo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja na imegawanyika katika sehemu mbili ya vitabu na ile ya kutumia mtandao ambapo wanafunzi wanasoma baada ya kuwashiwa mtandao huo.

Amesema chuo hicho pamoja na tawi lake lililopo  jijini Mwanza  kinatoa kozi  muhimu ambazo ni rafiki kwa ajira  huku akizitaja baadhi kuwa ni kozi za  Shahada ya kwanza ya Mipango ya Maendeleo ya mikoa, Shahada ya kwanza ya Mipango na Usimamizi wa Mazingira, Shahada ya kwanza ya Mipango na Maendeleo ya Jamii, Shahada ya kwanza ya Idadi ya Watu na Mipango ya Maendeleo, Shahada ya Juu ya Fedha za Maendeleo na Mipango ya Uwekezaji.

Makumu huyo amezitaja kozi nyingine kuwa ni Shahada ya kwanza ya Uchumi na Maendeleo, Shahada ya kwanza ya Mipango ya Biashara na Usimamizi, Shahada ya kwanza ya Maendeleo ya Miji na Usimamizi wa Mazingira, Shahada ya kwanza ya Mipango na Usimamizi wa Rasilimali Watu na Shahada ya kwanza ya Mipango na Usimamizi wa Miradi.




Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU