TOTAL INDUSTRIAL SOLUTIONS MKOMBOZI KWA WAWEKEZAJI WA VIWANDA

Na Asha Mwakyonde

WAWEKEZAJI na wajasiriamali wametakiwa kuchangamkia fursa ya kumiliki kiwanda ndani ya miezi sita kuanzia shilingi milioni 6 hadi 600 kwa wanaotaka kuwekeza kwenye viwanda.

Akizungumza  Julai 6 katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  kwa niaba ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko kutoka  Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO),Dk. Sigisbert Mmasi amesema wamekuja na Miliki kiwanda ndani ya miezi sita kuanzia shilingi milioni 6 hadi 600.

"Tumekuja kivingine  tumekuja kuwaambia watu ' Miliki kiwanda ndani ya miezi sita kuanzia shilingi milioni 6 hadi 600 yote haya yanawezekana katika banda la Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara.Tumekuja na kitu kinachoitwa Total Industry solutions ni suluhisho la kuwawezesha wajasiriamali ambao wanataka kuwekeza kwenye viwanda," amesema Dk.Mmasi.

Amesema kuwa katika banda hilo wana kitu kinaitwa Biashara Kiliniki  mjasiriamali anayetaka kuwekeza katika kiwanda anaweza akawa anawazo hana pesa ya kuwekeza akawa na kiwanda lakini hakifanyi vizuri akataka kukiendesha kwa tija hivyo Biashara Kiliniki inahusisha taasisi zote zitakazo mwezesha mjasiriamali kumiliki kiwanda.

Dk. Mmasi amesema kuwa nje ya banda la Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kuna taasisi nne amabazo zina viwanda huku akizitaja baadhi  kuwa ni Shirika kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania(TIRDO).

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA