Watu mbalimbali wakijifunza kutoka kwa wanafunzi wanaosomea fani ya umeme jua katika Chuo cha Ufundi Don Bosco.
Na Sifa Lubasi
KONGAMANO la career fair 'haki kazi' limefanyika katika Chuo cha Ufundi lDon Bosco Jijini hapa huku wanafunzi wakitakiwa kuwa wabunifu Ili waweze kunufaika na fursa za ajira zinazotolewa katika Taasisi za Serikali na zisizo za Serikalii.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Chuo hicho Dk Justine Mulebya wakati wa kongamano la “Career Fair” kwa mwaka 2022 lililofanyika Chuo hapo Miyuji Dodoma.
Alisema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wabunifu na wenye weledi Ili kubaini soko la ajira linataka nini.
Alisema kuwa wanafunzi wanatakiwa kusoma Ili watoe mchango wao kwenye jamii.
"Apate cheti kwa ajili ya kwenda kujiajiri au kuajiriwa na kwenda kutoa huduma kwa kile alichojifunza Ili watu wengine wanufaika nacho tunapenda kuona wanafunzi wanaotoka hapa na kwenda kuajiriwa au kujiajiri wanakuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza Chuo," alisema.
Pia alisema muhula wa masomo wa Septemba mwaka huu Chuo hicho kitaanza kutoa mafunzo.ya kozi mpya ya hoteli na utalii ngazi ya diploma.
Alisema katika kozi hiyo watatachukua wanafunzi wa kidato cha nne' wenye ufaulu wa alama D nne' na wale wa kidato cha sita wenye principle pass moja na subsidiary moja.
Aidha. alisema kozi nyingine mpya ni ile ya ualimu wa Ufundi.
Mmoja wa wadau waliohudhuria kongamano hilo Wilington Maleya ambaye ni Meneja wa Dodoma hotel alisema wamekuwa wawekezaji kwenye masuala ya hoteli ambapo sasa wanamiliki hoteli 19.
"Nina vijana 19 niliowaajiri kutoka Don Bosco kwenye fani za ufundi bomba na umeme, ukiajiri vijana wa hapa hutajuta lakini nashauri Chuo kiwe na kitengo cha kuwafuatilia wanafunzi wao wajue huko walipo wanafanya nini, sijawahi kuona mtu kutoka chuoni aje awatembelee, vijana wake' alisema.
Mdau mwingine Bakari Mmari alisema kuwa ana karakana ya Ufundi magari na amekuwa akipokea wanafunzi kutoka Chuo cha Don Bosco kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
" Kwa miaka mingi nimekuwa nikifanya kazi na hiki Chuo, wanafunzi wanatakiwa kuongeza umakini wanapokuwa kipindi cha kujifunza kwa vitendo Ili wanapomaliza ajira ziwatafute," alisema.
Mdau kutoka Simu Solar,Hadija Selemani alisema kuwa wamekuwa walipokea vijana kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na wamekuwa wakifanya kazi vizuri.
Mkurugezi wa Chuo hicho,Padri Boniface Mchami alisema kuwa Chuo hicho kimekuwa kinatoa kozi mbalimbali za ufundi ikiwemo ufungaji umeme, nishati ya jua na umeme, kuchomelea, Ufundi magari,uashi, Ufundi bomba, chakula na vinywaji, utayarishaji wa vyakula na kilimo ubunifu na teknolojia.
Mratibu wa mafunzo na malezi wa vijana katika Chuo hicho Anansia Lema alisema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuwaunganisha vijana na wadau walio kwenye soko la ajira .
"Hapa wamekutana na wadau mbalimbali ambao huwa wanatoa ajira hili litawawezesha kuajiriwa au kujiajiri kwa urahisi," alisema.
Nicodemus Mtende ambaye ni mmoja wa wanafunzi walionufaika na mradi wa umeme jua kutoka Kampuni ya IMED foundation alisema kuwa walipata kozi fupi kuhusiana na masuala ya umeme jua.
"Kila mwanafunzi aliandika wazo la biashara na waliofaulu walipewa vifaa vya kufanyia kazi kulingana na wazo aliloandika," alisema.
Fabiano Mugune alisema kuwa baada ya shindano hilo alishinda na kupatiwa mashine ya kutotolesha vifaranga ambayo inatumia umeme wa jua.
" Mashine hiyo ina uwezo wa kutotolesha mayai 112, imekuwa ni msaada sana kwangu kwani imemuwezesha kujiajiri kwa kuuza vifaranga," alisema.
Aliwataka vijana ambao hawakubahatika kuendelea na elimu ya juu kujiunga kwenye vyuo vya Ufundi kwani kuna fursa nyingi za ajira.
0 Comments