TEMDO YAJA NA TEKNOLOJIA MPYA YA KITEKETIZI TAKA ZA HOSPITALI


 Na Asha Mwakyonde

TAASISI ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO),imebuni kiteketizi cha taka nguvu za  hospitali  kitaaluma huitwa Health care Solid Weste Incinerator, ambacho kina uwezo wa kuchoma taka hatarishi na ni salama kwa mazingira ya afya ya mwanadamu.

Pia TEMDO inawakaribisha wenye vituo vya afya, hospitali kupeleka mahitaji yao ili waweze kutengenezawa kwa kuwa lengo lake ni kubuni Teknolojia hivyo hata kama Teknolojia hiyo haipo katika taasisi kwa kuwa inawahandisi wabobezi wakutosha wenye uwezo wa kubuni bidhaa mbalimbali kulingana na mahitaji ya mteja.

Akizungumza Julai 6 katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko  kutoka TEMDO, Dk. Sigisbert Mmasi amesema kuwa kiteketizi hicho kina chemba mbili ya kwanza inasaidia joto lake linafika 500 hadi 600.

Dk. Mmasi amefafanua kuwa taka hizo zinazochomwa na moshi unapanda unaenda juu chemba ya pili  na kwamba moshi huo unatoka chemba hizo utakuwa hauna madhara kwa binadamu.

" Wataalamu wanasema taka za hospitali zikichomwa katika joto dogo ni hatari kwa afya hivyo wanashauri zichomwe katika joto kubwa la nyuzi 1000 ambapo haitakuwa na  madhara ya kiafya kwa binadamu," amesema.

Mbali na kiteketizi hicho Dk. Mmasi amesema kuwa TEMDO ina vifaa tiba mbalimbali vikiwamo vitanda kwa ajili ya mapokezi, kulazia wagonjwa, na vile vya kujifungulia akina mama.

" Tumebuni vifaa 16 tunatarajia Disemba mwaka huu tutakuwa tumetoa aina nyingine ya vifaa tiba. Tunawakaribisha wenyewe vituo vya afya, Hospitali  waweze kuleta mahitaji yao ili TEMDO iweze kuwatengenezea.

TEMDO ni taasisi ambayo ipo chini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara na baadhi ya majukumu yake ni kufanya tafiti na kubuni mashine za aina mbalimbali za kutumika katika viwanda vidogo,vya kati na vikubwa pamoja na kutoa huduma za kiuhandisi na kutoa mafunzo kwa wahandisi.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA