MOI YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO

 

Daktari Bingwa wa Mifupa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk. Sharifu Luena akimpa maelekezo ya huduma zinazopatikana katika taasisi hiyo mteja aliyetembelea banda hilo.

Na Asha Mwakyonde

DAKTARI Bingwa wa Mifupa  kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI), Dk. Sharifu Luena amesema kuwa katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba yanayaofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere taasisi hiyo imeluja na huduma za kibingwa ambazo zinapatikana MOI.

Akizungumza Julai 6,2022 katika Maonyesho hayo Dk. Luena amesema kuwa wananchi wote wanaotembelea banda la MOI wanapata nafasi ya kuonana na madaktari wa Mifupa na Ufahamu yaani Ubongo na kwamba wanawasaidia wateja wao pamoja na kuwapatia ushauri kulingana na tatizo la mteja wao.

" Maonyesho haya ya mwaka huu tunapatikana katika banda la Jakaya Kikwete tumekuja na watu wa mazoezi tiba na wataalamu wa viungo bandia na kwa wale wenyewe shida ya mgongo, maumivu ya mgongo ya muda mrefu na waliopata ajali kwa bahati mbaya wakakatwa viungo wanaweza wakaja kuonana na wataalamu hawa kwa ajili ya matibabu zaidi," ameeleza Dk.Luena.

Ameeleza kuwa taasisi hiyo imejikita zaidi katika huduma za kibingwa za Mifupa, tiba ya Ufahamu yaani Ubongo na Uti wa mgongo.

Daktari huyo ameongeza kuwa katika banda hilo wanawatalamu wa lishe hivyo wananchi wanakaribishwa kupima urefu na uzito pamoja na kupatiwa ushauri bure.
 

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA