NIDA YAWATOA HOFU WATANZANIA


Na Asha Mwakyonde

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa( NIDA),imewatoa hofu Watanzania kutokana na vitambulisho vya Taifa vya mwaka 2012  kuonesha vinaisha muda wake  huku ikiwatakwa kuendelea kutumia  kuwa utambulisho wao utabaki palepale.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Msemaji wa Mamlaka hiyo Geofrey Tengeneza alisema kinachokwenda kuisha muda wa matumizi ni kibebeo cha kitambulisho lakini utambulisho wa mwanachama unabaki palepale.

Alisema huduma zote ambazo wamekuwa wakizipata kupitia kitambulisho hicho au namba ya kitambulisho utabaki kuwa palepale licha ya muda wa kitambulisho kwenda kuisha.

" Licha ya kwenda kuisha kwa muda wa matumizi ya kibebeo cha kitambulisho cha taifa naomba Wananchi mjue kuwa utambulisho wa mwananchi unapaki pale pale na auishi muda wa matumizi"alisema

Tengeneza alisema kinachokwenda kufanyika baada ya muda kuisha muda wa kitambulisho mwananchi atapaswa kwenda katika ofisi ya wilaya katika eneo ambalo anaishi kufika pale kwa ajili ya kupigwa picha.

"Zoezi ambalo litafanyika ni kupiga picha tu hakutakuwa na hatua uhakiki wa taarifa zako na baada ya hapo NIDA tutaendelea utaratibu wa kuandaa kanzi data yetu"alisema

Aliendelea kufafanua kuwa matumizi ya kitambulisho cha taifa yamekuwa ni ya miaka 10 lengo likiwa ni kufanya mabadiliko ya taarifa  za Wananchi tofauti na zile ambazo alitoa awali.

Akitaja sababu za kufanya mabadiliko ndani ya miaka 10 Tengeneza alisema inawezekana mtu akawa amebadilisha makazi ya awali hivyo ni lazima  taarifa zake zikahuishwa katika mfumo wa kanzi data.

Pia alisema katika muda wa miaka 10 muonekano wa mtu  unaweza ukawa umebadilika hivyo katika kipindi hiki ni lazima afanye mabadiliko .

"Hizi ndizo sababu ambazo kwanini tumeweka muda wa miaka 10 nawaomba watanzania wasiwe na hofu yoyote Wala kuhusu foleni pindi mchakato utakapoanza wa kupiga picha hakutakuwa na foleni ya aina yoyote endapo hatakuwa na taarifa za kuhusisha,"alisema.

Vilevile alisema  vitambulisho hivyo ambavyo ni vya mwaka 2012 avitakuwa vikiisha muda mmoja na badala yake vinaisha kwa muda tofauti kulingana na tarehe na mwezi na mwaka hivyo Wananchi wasiwe na hofu kuhusu suala la foleni.

Aidha alisema NIDA imejipanga kutoa huduma hiyo kwani tayari imekwisha toa oda ya vifaa vipya kwa ajili ya zoezi hilo.

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA