VETA MOSHI YABUNI KIFAA CHA KUPUNGUZA UMEME


Mwanafunzi wa chuo cha ufundi stadi Moshi Disimas Masawe akionyesha na kuelezea namna ya  kifaa cha Programmable Logic Controller kinavyofanya kazi.

Na Asha Mwakyonde

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia chuo Ufund Stadi VETA,Moshi imekuja na kifaa cha Programmable Logic Controller (PLC),ambacho kinapunguza matumizi ya umeme majumbani ambapo taa zinajizima baada ya muda fulani kuwashwa.

Akizungumza  Julai 5, ,2022  katika banda la VETA  kwenye Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba Mwanafunzi Mbunifu wa mwaka wa pili katika chuo cha ufundi stadi Moshi Disimas Masawe amesema lengo la kifaa hicho ni kupunguza matumizi ya umeme majumbani.

" Mara nyingi katika vyumba ya kulala kunakuwa na swichi mbili lakini kifaa hiki kitasaidia kupunguza swichi kwani mtu anapoingia chumbani kwake na kuwashwa taa atakapomaliza shughuli za kutandika na kulala inajizima yenyewe,' amesema Masawe.

Amesema wakati wa usiku taa zinatumika kuwaka muda mwingi  hivyo wameona wapunguze gharama huku akitole a mfano mtu anapotoka sebuleni kwenda chumbani taa ya sebuleni inajizima na atakapofika chumbani inajiwasha.

Masawe ameongeza kuwa Jokofu huwa linawashwa muda mrefu lakini kupitia kifaa hicho mtumiaji anaweza kutengeneza kizime baada ya masaa matatu au manne kutokana na matumizi yake halafu baadae kinawaka tena.

Ameeleza kuwa kifaa hicho mara nyingi kinatumika viwandani hivyo ameona  ni vema kikatumika hata nyumbani ili kumpunguzia gharama  za umeme mwananchi.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI