Mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe Nelson Sanga akielezea namna mkojo wa Sungura unavyoweza kutumika kama mbadala ya kemikali kwenye kilimo cha mboga mboga na matunda.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na Masoko kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Rose Joseph (Kushoto), akijadiliana jambo na Maofisa wa chuo hicho katika banda lao (Kulia), ni Mratibu wa Udahili Dk. Michael Mangula na (Katikati), ni Afisa Udahili Isaac Msengi.
Na Asha Mwakyonde
CHUO Kikuu Mzumbe kimekuja na mkojo wa Sungura kama njia mbadala ya kilimo cha mboga mboga na matunda badala ya kutumia kemikali kupulizia lengo likiwa ni kuokoa afya za watumiajia wa matunda na mboga mboga hizo.
Akizungumza Julai 4,2022 katika banda la chuo hicho kwenye Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba Mwanafunzi wa Mzumbe Nelson Sanga amesema kuwa kazi ya mkojo huo hutumika kama kemikali mbadala kwenye kilimo cha mboga mboga na matunda.
Mwanafunzi huyo ameeleza kuwa mfumo wa ulaji kwa jamii umeanza kubadilika Kwa sasa watu wanatumia vyakula vya asili ni kutokana na magonjwa mengi ambayo yanawasumbua.
"Lengo kubwa katika maonyesho haya ni kuonyesha Umma mkojo huu unavyotumika badala ya kemikali katika kupulizia mboga mboga na matunda. Mkojo huu unachanganya na maji kiasi kabla ya kupulizia katika kilimo hiki," amesema.
Ameongeza kuwa mkojo huo una harufu kali ambao hauruhusu wadudu kushambulia mboga na matunda huku akisema kwa matumizi ya binadamu hauna shida.
Sanga amefafanua kuwa hiyo ni fursa nzuri kupitia mkojo huo kwani mfugaji wa Sungura anaweza kuongeza mnyororo wa thamani na kwamba lita moja inauzwa shilingi 12,000 hadi 15,000.
Amesema hakuna changamoto yoyote katika ufugaji wa Sungura mkulima anachotakiwa kufanya ni kujenga sehemu nzuri ya kuelekezea mkujo huo wakati wa kukusanya.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano na Masoko kutoka chuo hicho Rose Joseph ambaye pia ni Msiamamizi na Mratibu banda hilo amesema lengo la kituo hicho pamoja na kufanya tafiti mnalimbali ni kuwajengea uwezo vijana ili kuwa na viti ambavyo vitawasaidia kufanya bunifu na baadae waweze kujiajiri.
" Tumekuja na bunifu mbalimbali ambazo zinahusisha wanafunzi ambao mawazo, bunifu zao kutokana na kituo chetu kuatamia mawazo ya wanafunazi. Lengo letu ni namna ya kuisaidia serikali ambayo inapambana na tatizo la ajira kwa vijana," ameeleza Rose.
Ameongeza kuwa wanafunzi kumaliza chuo na kusubiri ajira hiyo dhana imepitwa na wakati na kwamba chuo hicho kinajitahidi tangu mwanafunzi anapoingia chuoni kuanzia wazo, kufikiri, kuja na miradi na mapendekezo ambayo Wataalamu wao wabobezi kwenye masula ya vifungashio wanaweza kuwasaidia vijana hao kupanua mawazo yao na kuanza kubuni mradi na Teknolojia ambayo itatatua changamoto kwa jamii.
0 Comments