TPDC YAJIVUNIA KUONGOZA KULIPA KODI


 Na Asha Mwakyonde

SHIRIKA  la Taifa ya maendeleo ya mafuta Na gesti tanzania (TPDC),limekuwa shirika la Umma linaloongoza kwa  ulipaji Kodi hapa nchini ambalo pia  lina simamia miradi mikubwa  mitatu.

Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa eyasiwembere ambao  ni mradi  wa mafuta na gesi asilia,bomba lá mafuta eacop na gesi Asilia ya lng.

Hayo yamesemwa Julai 4, 2022 katika banda la TPDC kwenye maonyesho ya 46 ya kimataifa ya wafanya biashara maarufu sabasaba na Afisa uhusiano wa  Shirika hilo,Francis Lupokela amesema wanajivunia kuwa walipaji kodi wakubwa.

Amesema ulipaji kodi kwa wakati umewawezesha kushiriki maonyesho hayo ili kuwaonesha wananchi kazi zinazofanywa na shirika hilo huku akisema asilimia 62 sawa na megawat 1021.32 ya umeme wa majumbani hapa Tanzânia  unatumia gesi ndio watafutaji wakubwa wa gesi na mafuta.

Afisa huyo amesema kwa sasa nyumba 1500 zinatumia gesi asilia viwanda 48,taasisi za kiserikali 2 gereza lá keko na chuo kikuu chá dar és salaam.

" TPDC pia inatoa huduma ya gesi Asilia kwa serena hoteli,taasisi nne za serikali ziliopo mtwara na zaidi ya magari 1400 hapa nchini yanatumia gesi hii ,"amesema lupokela.

Ameitaka serikali kuendelea kuwaamini katika suala zima lá ufanyakazi kwa kuwa wapo kwa ajili ya kuipa heshima na hadhi kubwa nchi ya Tanzânia kwa kukamilisha miradi kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI