VETA DODOMA YABUNI MTAMBO WA KUZALISHIA GESI

Mbunifu Asia Shabani akionyesha  namna Mtambo huo unavyofanua kazi.

Na Asha Mwakyonde

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), kupitia chuo Ufund Stadi i VETA, Dodoma kimebuni Mtambo wa kuzalishia gesi kwa kutumia jiko la gesi ambao unatumia petroli na maji ikiwa ni Kuendeleza kauli mbinu ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji na biashara.

Akizungumza Julai 4,2022  katika banda la VETA  kwenye Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba Mwanafunzi Mbunifu  wa mwaka wa pili Asia Shabani amesema lengo kubuni mradi huo ni kupunguza matumizi makubwa ya gesi na kufanya matumizi yake kuwa rahisi kwa kila mtu. 

" Mtu anaweza kutumia Mtambo huu katika biashara kama vile mama lishe,Hospitalini , sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi, na hata majumbani," amesema Asia.

Ameongeza kuwa Mtambo huu unaweza kutoa ajira kwa vijana kwa kusambaza gesi itakapotokea kimepatikana kibali cha kujaza gesi.

Mbunifu huyo akizungumzia changamoto za wanazokutana nazo kama wabunifu ni ukosefu wa vifaa na sapoti kutoka kwa walimu wao ambapo kwa sasa wanachangishana fedha kwa lengo la kutengeneza vitu mbalimbali ili Kuendeleza ujuzi wao.

Ameeleza kuwa hadi kukamilika kwa Mtambo huo wametumia gharama ya fedha kiasi cha shilingi 150,000 ambapo watakiuza shilingi 300,000 kitakapotishwa na Mamlaka husika.

Mbunifu huyo amewataka vijana kwenda kutembelea banda la VETA ili kuona bunifu mbalimbali zinazofanywa na vijana wenzao.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI