BRELA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA MABANDA YAO SABA SABA

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Roida Andusamile ( kushoto),akimkabidhi cheti cha usajili wa majina ya biashara mmoja wa watu waliofika katika moja ya banda hayo.

Na Asha Mwakyonde

MKUU wa cha Habari na Mawasiliano kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA),Roida Andusamile amesema moja ya faida ya kurasimisha biashara kwa wafanyabiashara, wajariamali ni kuwa katika mazingira bora na salama ya ufanyaji biashara na tayari zaidi ya watu 300 wamerasimisha biashara zao.

Haya ameyasema Julai 4,2022 wakati akizungumza katika moja ya mabanda yao kwenye Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Saba Saba, Roida amesema kuwa kila mwaka BRELA inashiriki maonyesho hayo lengo likiwa ni kuhamasisha wadau kwenda kurasimisha biashara zao ili kuondoa vikwazo mbalimbali kwa wafanyabiashara.

"Tunaporasimisha biashara tunatoa majina ya biashara, majina, ya kampuni, alama za biashara na huduma tunatoa leseni za kundi A za viwanda  na tunasajili viwanda vidogo na huduma zote hizi tinazitoa hapa BRELA," amesema Mkuu huyo wa Kitengo.

Ameeleza kuwa lengo la kutoa huduma hizo ni kuhakikisha mfanyabiashara anakuwa katika mazingira mazuri na kwamba kwenye maonyesho hayo wanatoa usaidizi wa karibu kwa wafanyabishara ambao wamekwama wanaotaka kusajili kwa njia ya mtandao.

" Lazima mfanyabisha anayehitaji huduma hizi awe na barua pepe ili aweze kuingia katika tovuti ya BRELA na kufanya maombi ya usajili. Maonyesho haya yamekuwa fursa kwetu kwani  zaidi ya watu 300 weshasajili biashara zao tangu maonyesho yaanze," amesema Andusamile.

Mkuu huyo wa Kitengo cha mawasiliano amesema kuwa wanawahamasisha wafanyabishara, wajasiriamali amabo bado hawajafika katika mabanda yao mawili  moja ambalo lipo nje ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango na jingine lililopo ndani ya banda la Uwekezaji, Viwanda na Biashara yote yanayoa huduma hizo za usajili.

Aidha amewakaribisha wananchi kutembelea mabanda hayo ya BRELA ili kurasimisha biashara zao huku akisema gharama za usajili wa majina ni 20,000 na Kwa upande wa kampuni inategemea na aina ya mtaji wa mfanyabiashara.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU