VETA YAJA NA MASHINE YA KUKAUSHA VITUNGUU, MATUNDA


 Mashine ya kuchakata matunda na viungo na  kuwa katika mfumo wa unga ili kumsaidia mkulima kuhifadhi mazao yasiharibike kwa muda mrefu.

Na Asha Mwakyonde 

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),imekuja na ubunifu mpya wa mashine ya kuchakata matunda na viungo kwa kuwa  katika mfumo wa unga ili kumsaidia mkulima kuhifadhi mazao yasiharibike kwa muda mrefu.

Mashine hiyo ina sehemu tatu ambazo kila moja ina kazi yake ya kwanza ni  kukatakata viungo au matunda tayari kwa kuyakausha kwenye machine nyingine ndogo na baada ya hapo inaingia kwenye mashine ya kusaga kuwa unga

Haya yamesemwa na Mbunifu wa mashine hiyo George Nyahende wakati akizungumza kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam,katika banda la VETA ameeleza kuwa aliona wakulima hasa maeneo ya vijijini wanapata hasara hivyo mashine hiyo itawasaidia kukusha mazoa yao na kuyahifadhi. 

Ameaema mashine hiyo ni nyenzo bora na  ya kisasa inayomsaidia mkulima  mjasiriamali kuchakata mazao na kuyaongezea mnyororo wa thamani huku akitole mfano wakulima wa vitunguu ambapo soko muda mwingine linakuwa shida hivyo wataweza kuvikausha na kuhifadhi unga.

" Mashine hii wakulima  wakitumia wanavikausha vitunguu na kuvisaga na kuwa unga na hapo watahifadhi kwa muda mrefu huku wakisubiri Soko ,"amesema Nyahende.

Mbunifu huyo ameongeza kuwa lengo la kubuni mashine hiyo ni kutokana na fursa ya maeneo mengi ya vijijini  kuwa na   umeme wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA),ambao umesambazwa  maeneo hayo hivyo wakulima wanaweza kununua mashine hiyo na kuondokana na umaskini.

Moja ya mashine hizi  ni ya kukausha matunda,viungo au nyama hutumia muda kati ya saa sita hadi 12 kulingana na bidhaa na baada ya hapo unasaga na kupata unga kisha unaweza kuufungasha kwa ajili ya kuhifadhi," amesema Nyahende.

Akizungumzia gharama ya  seti ya mashine hiyo ni shilingi milioni moja na ina muda wa matazamio kwa mteja wa mwaka mmoja baada ya kuinunua huku akisisitiza kuwa ina ubora na malighafi zilizotumika kutengeneza zimetoka hapa nchini.

pia Mbunifu huyo awamewashauri wajasiriamali, vikundi vya wajasiriamali wanaweza kuinunua na kuitumia kuzalisha bidhaa zao kwa kuwa inamatokeo mazuri na yenye viwango vya ubora.

Ameeleza kuwa wapo katika banda la VETA kutoa elimu kuhusu mashine hiyo linavyotumika hivyo amewataka  wajasiriamali na wananchi kutembelea banda hilo kwa lengo la kupata uelewa zaidi.

 


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI