KATAMBI AWATAKA VIJANA KUJITAMBUA NA KUJITUMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

 

Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Patrobas Katambi katika  Kongamano la Vijana la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Vijana.

Baadhi ya Vijana walioshiliki katika Kongamano la Vijana la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Vijana.

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu Patrobas Katambi,  amewataka vijana kujitabua ,kuwa na uthubutu pamoja na kujiwekea malengo pamoja na kujituma kufanya kazi.

Hayo ameyasema Oktoba 28, 2022 jijini Dodoma Wilayani Chamwino katika Kongamano la Vijana la fursa zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Vijana,
Katambi mesema lengo la Kongamano hilo ni kumwezesha kijana kujitambua na atambue nafasi yake kwenye Jamii,

Ameongeza kuwa Vijana wengi wanafikra ya utegemezi hawataki kufanya kazi hawataki kujituma, Amesema Kama mnavyofahamu, vijana duniani kote ndio wanaochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza na kujenga uchumi wa mataifa yao. 

Katambi amefafanua kuwa kila kijana anatakiwa kupambana kivyake  na kukumbuka Serikali yetu ni moja huku akiwasisitiza vijana  ha kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

"Ili tuwe na Taifa lenye Nguvu tunahitaji Vijana wachapakazi wanao jituma hata vitabu vya dini vimewataka vijana kufanya kazi” ameongeza.

Huwezi kupewa lifti kama umekaa nyumbani wakati unasafari ya kwenda Dar es Salaam lazima usogee Barabarani ukisimama tu wanajua wewe ni msafiri utapewa lifti," ameeleza Katambi.

Kwa upande wake Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora, Deogratius Ndejembi amewasisitiza vijana kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali .

Amesema Serikali ya hawamu ya sita imejipanga kutokomeza dibwi la vijana wasio na kazi za kufanya, wasio na Ajira.

"Ajira inaweza ikawa kwenye kilimo inaweza kuwa kwenye mifugo au kwenye pikipiki (Boda boda) na mama lishe, ndiyo maana tumekutana hapa kwa lengo la kujengeana kupitia haya mafunzo yanayotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Vijana, " amesema.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Gift Msuya amewapongeza Vijana kwa kuwa na mwitikio mkubwa wa kujitokeza zaidi ya vijana 300 ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali namna ya kupambana na fursa tunataka Vijana wajiajiri wenyewe.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI