WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA UTAMADUNI WA KULA NYAMA


NA ASHA MWAKYONDE,DODOOMA

MSAJILI wa bodi ya nyama nchini Dk. Daniel Mushi amewasisitiza Watanzania kujenga utamaduni wa kula nyama ili kukabiliana na utapiamlo.

Ametoa kauli hiyo wakati  akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa habari maelezo Jijini Dodoma amesema  utafiti unaonyesha Mtanzania mmoja hula kilo 15 za nyama kwa mwaka  badala ya kilo 50 kama inavyotakiwa ambapo katika baadhi ya nchi za Ulaya na nyinginezo mtu mmoja anakula kilo 100 kwa mwaka.

Aidha,amepinga kauli ya watu kuwa nyama nyekundu ni hatari bali mlaji anatakiwa kuandaa nyama vizuri kuanzia katika kuipika hadi kwenye ulaji.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa kwa sasa wana mipango thabiti ya kutafuta masoko ya uhakika kwani mahitaji ya nyama nje ya nchi ni makubwa lakini Tanzania inasafirisha nyama kwa kiwango kidogo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI