MAANDALIZI YA UWANJA KWA AJILI YA KUTANGAZA MATOKEO YA AWALI YA SENSA YANAENDA VIZURI



Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah akizungumza katika Uwanja wa  Jamhuri alipotembelea na  kukagua maandalizi ya Uzinduzi wa Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022 unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31,2022 Jijini Dodoma.

NA ASHA MWAKYONDE, DODOOMA

MAKAMU  wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah  amesema maandalizi ya uwanja wa Jamuhuri kwa ajili ya kutangaza matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi  ya mwaka 2022 yamefikia asilimia 85.

Rais Samia Suhuhu Hassan anajarajiwa kutangaza matokeo hayo Oktoba 31 mwaka huu pamoja na kuzindua Muongozo wa matumizi wa matokeo ya Sensa hiyo ambayo imefanyika Agosti 23 mwaka huu.

Akizungumza  jijini Dodoma Oktoba 29, 2022 katika Uwanja wa Jamhuri alipotembelea na  kukagua maandalizi ya uzinduzi wa matokeo ya Sensa hiyo Makamu huyo wa Rais amesema kuwa kilichobakia ni maandalizi madogo madogo na kwamba hadi kufikia kesho uwanja huo utakuwa umeshakamilika.

Makamu huyo  wa pili wa  Rais wa Zanzibar Abdullah ameeleza kuwa Rais Samia atazindua matokeo hayo ya Sensa ya awali na kwamba wamejipanga vizuri kwa kuwa sensa ya mwaka huu ni ya kidigitali hivyo hata maandalizi yake ni tofauti na miaka iliyopita.

Ameongeza kuwa matokeo hayo yataoa dira ya mwelekeo wa serikali katika kupanga mipango yake ya kimaendeleo baada ya kupata takwimu sahihi.

Aidha amewashukuru Watanzania wote kwa kushirikiana na serikali yao hadi kufikia hatua  ya kuyatangaza matokeo hayo huku akiwashukuru pia waandishi wa habari kwa kazi kubwa walioifanya ya kuhabarisha Umma kuhusu Sensa hiyo.




Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU