WAFANYABIASHARA PWANI WAASWA KUJIUNGA NA JWT


NA MWANDISHI WETU PWANI

KATIBU  Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiasha Mkoa wa Pwani (JWT),Wellu  Mtaki amewataka wafanyabiashara wa mkoa wa pwani kujiunga na jumuiya ya wafanyabiashara  kwa ajili ya kunufaika na fursa zilizopo katika jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa na Katibu huyo wakati wa mahojiano na Vyombo vya habali mkoani pwani kuhusu utekekezaji wa majukumu ya taasisi hiyo Pamoja na fursa zilizopo ndani ya jumuiya.

Amesema jumuiya inamwezesha mfanyabiashara kutatua changamoto yake Kwani mfanyabiashara  huyo anauwezo wa  kutoa kero, maoni na maoendekezo  yanayohusu biashara na taasisi ikafikisha sehemu husika kwa ajili ya Utatuzi  tofauti na mtu kupeleka kero yake mwenyewe.

" Lengo la jumuiya ni kuwaunganisha kwa Pamoja wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katika  eneo la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwawezesha kutoa mawazo na maoni yao kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabishara KWa nia ya kuwakilisha serikalini" amesema Mtaki

Aidha Mtaki amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kutengeneza mazingira bora ya kufanya biashara nchini Tanzania huku akifafanua kuwa huduma ya bima kwenye taasisi hiyo imeaza kutolewa KWa wafanyabiashara ambao wamejiunga na Jumuiya hiyo.

" Huduma za bima zinazotolewa ni Pamoja na bima ya Elimu au Carrier Life Plan kipitia shirika la bima la jubilee ambalo linamsaidia mtoto wako kunufaika mahitaji yake ya elimu , pia Bima ya Afya ambayo  ina kifurushi cha aina tatu ambacho Scare individual and Family health insurance, Pamoja Afya, Jubilee Afya na huduma ya Bima ya Nafaka" amesema Mtaki.

Pia Mtaki ametoa wito kwa wafanyabiashara wote mkoa wa pwani kuhakikisha wanafata taratibu na muongozo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TLA ),ili kuepuka Changamoto zitakazojitokeza.

Ikumbuke Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania haijihusishi wala kufungamana na udini, ukabila, siasa, wala ushabiki wa michezo na mambo yanayofanana na hayo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI