Na Asha Mwakyonde, DODOMA
UONGEZAJI thamani wa mazao ya nyuki umeendelea kuwa chanzo cha ajira na fursa za biashara kwa vijana nchini, huku matumizi ya bidhaa za asali yakiongezeka kutokana na kuimarika kwa uelewa wa wananchi kuhusu faida zake kiafya.
Mmiliki wa bidhaa za nyuki, Noreen Banyema maarufu Bee Blessing, amesema sekta hiyo imemwezesha kujiajiri, kuajiri wengine na kupanua masoko kupitia ubunifu wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao ya nyuki.
Akizungumza katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane 2026 kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT), chini ya Wizara ya Kilimo, Bee Blessing amesema anajishughulisha na uzalishaji, ununuzi na uongezaji thamani wa mazao ya nyuki kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu.
Bee Blessing amezitaja bidhaa hizo kuwa ni asali ya nyuki wadogo, asali ya nyuki wakubwa, chavua ya nyuki (bee pollen), maziwa ya nyuki (royal jelly),asali ya viungo, tangawizi pamoja na bidhaa ya mixed nuts inayochanganya karanga, korosho, almond na mbegu za maboga na kuongeza asali mbichi pamoja na bee pollen.
Ameeleza kuwa asali ya viungo hutengenezwa kwa kutumia viungo vinavyolimwa nchini kama tangawizi, karafuu na mdalasini, hivyo kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na kutoa bidhaa yenye virutubisho vingi inayoweza kutumika kama kiongozea cha chai na kwa ajili ya afya.
Aidha,amesema bidhaa za asali hazitumiki kwa chakula pekee, bali pia hutumika katika utengenezaji wa sabuni, mafuta na bidhaa nyingine za urembo zinazotumia asali halisi kama malighafi.
Bee Blessing amesema mahitaji ya bidhaa za nyuki yameendelea kuongezeka kwa kasi kadri wananchi wanavyoelewa umuhimu wa asali na mazao mengine ya nyuki, huku wengi wakipunguza matumizi ya sukari na kuelekeza matumizi yao kwenye asali asilia.
Ameongeza kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yamechangia kwa kiasi kikubwa kupanua soko la bidhaa zake na kuwafikia wateja wengi zaidi ndani na nje ya nchi.
Mmiliki huyo ameishukuru Serikali kwa kuanzisha Programu ya BBT iliyowawezesha vijana kushiriki katika Maonesho ya Nanenane huku akisema fursa hiyo imewasaidia kutangaza biashara zao,kujifunza na kuunganisha nguvu na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo.
Pia amewataka vijana kutumia fursa zilizopo katika kilimo, ufugaji na uongezaji thamani wa mazao badala ya kusubiri ajira rasmi, akieleza kuwa sekta hizo zina uwezo mkubwa wa kuzalisha kipato na ajira.
"Vijana wasisite kuuliza, kujifunza na kujenga mitandao ya kitaaluma na kibiashara. Pia watumie mitandao ya kijamii na kutembelea mara kwa mara tovuti za taasisi mbalimbali ili kupata taarifa za fursa zinazoweza kubadili maisha yao," amesema.
Ameshukuru sekta hiyo kwa kuwa imemsaidia kutoa ajira ambapo ameajiri vijana watatu wa kudumu katika kampuni yake na wengine wawili wa muda ambao wanafanya kazi kwa msimu.
Aidha, ameiomba Serikali kuendelea kuunga mkono wajasiriamali wa sekta ya nyuki kwa kuongeza uwekezaji na kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha sekta hiyo kukua zaidi na kuchangia uchumi wa Taifa.
BEE BLESSING: UONGEZAJI THAMANI MAZAO YA NYUKIWANIFUNGULIA AJIRA NA MASOKO
Na h Mwakyonde, DODOMA
UONGEZAJI thamani wa mazao ya nyuki umeendelea kuwa chanzo cha ajira na fursa za biashara kwa vijana nchini, huku matumizi ya bidhaa za asali yakiongezeka kutokanana kuimarika kwa uelewa wa wananchi kuhusu faida zake kiafya
Mmiliki wa bidhaa za nyuki, Noreen Banyema maarufu Bee Blessing, amesema sekta hiyo imemwezesha kujiajiri, kuajiri wengine na kupanua masoko kupitia ubunifu wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao ya nyuki.
Akizungumza katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane 2026 kupitia Programu ya Building a Better Tomorrow (BBT), chini ya Wizara ya Kilimo, Bee Blessing amesema anajishughulisha na uzalishaji, ununuzi na uongezaji thamani wa mazao ya nyuki kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu.
Bee Blessing amezitaja bidhaa hizo kuwa ni asali ya nyuki wadogo, asali ya nyuki wakubwa, chavua ya nyuki (bee pollen), maziwa ya nyuki (royal jelly),asali ya viungo, tangawizi pamoja na bidhaa ya mixed nuts inayochanganya karanga, korosho, almond na mbegu za maboga na kuongeza asali mbichi pamoja na bee pollen.
Ameeleza kuwa asali ya viungo hutengenezwa kwa kutumia viungo vinavyolimwa nchini kama tangawizi, karafuu na mdalasini, hivyo kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na kutoa bidhaa yenye virutubisho vingi inayoweza kutumika kama kiongozea cha chai na kwa ajili ya afya.
Aidha,amesema bidhaa za asali hazitumiki kwa chakula pekee, bali pia hutumika katika utengenezaji wa sabuni, mafuta na bidhaa nyingine za urembo zinazotumia asali halisi kama malighafi.
Bee Blessing amesema mahitaji ya bidhaa za nyuki yameendelea kuongezeka kwa kasi kadri wananchi wanavyoelewa umuhimu wa asali na mazao mengine ya nyuki, huku wengi wakipunguza matumizi ya sukari na kuelekeza matumizi yao kwenye asali asilia.
Ameongeza kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yamechangia kwa kiasi kikubwa kupanua soko la bidhaa zake na kuwafikia wateja wengi zaidi ndani na nje ya nchi.
Mjasiriamali huyo ameishukuru Serikali kwa kuanzisha Programu ya BBT iliyowawezesha vijana kushiriki katika Maonesho ya Nanenane huku akisema fursa hiyo imewasaidia kutangaza biashara zao,kujifunza na kuunganisha nguvu na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo.

0 Comments