TANROADS: MIRADI 44 KUGHARIMU TRILIONI 3.8

NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

JUMLA ya miradi 44 ya barabara yenye urefu wa Kilometa 1,523,  itatumia kiasi Cha Shilingi Trilioni 3. 8 ambayo ikihusisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa kupitia Washirika mbalimbali wa Maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Oktoba 29,2022 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) , Mhandisi, Rogatus Mativila wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wakala hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2022-2023,

Mhandisi huyo Ma ameeleza  kuwa mradi mkubwa wa ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Msalato unaojumuisha ujenzi wa njia ya kurukia ndege na majengo ya abiria unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 360.

Ameongeza kuwa mbali na miradi hiyo 44 iliyopo katika hatua mbali mbali ya ujenzi kuna miradi mingine 62 ya barabara iliyopo katika hatua za manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.

"Barabara hizi zipo katika hatua ya manunuzi zinajumuisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani pamoja na fedha kutoka kwa Washirika wa maendeleo,"amesema Mhandisi huyo.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI