NBS: IDADI KAMILI YA WATANZANIA KUJULIKANA MACHI 2023


 NA ASHA MWAKYONDE, DODOMA

MTAKWIMU  Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa yaTakwimu(NBS),Dk.Albina Chuwa amesema idadi ya watu 61,741,120 ni ya walio lala nchini usiku wa kuamkia siku ya sensa ambayo imefanyika Agosti 23 mwaka huu   bila kujali Utaifa wao.

DK.Chuwa amesema Matokeo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan ni ya mwanzo ikumbukwe kuwa dodoso la sensa lilikuwa na maswali 100, hivyo zitatolewa awamu kwa awamu na kwa namna tofauti.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa November 11,2020 Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk. Chuwa amesema Machi mwakani wakatoa chapisho lingine litakalo kuwa linaeleza watanzania ni wangapi katika idadi hii ya 61,741,120, litabainisha idadi ya watu kulingana na utaifa wao

Mtakwimu Mkuu huyo ameeleza kuwa
uchambuzi wa kina unaendelea ili kubaini watu walio lala nchini na utaifa wao huku akisema kwa sasa NBS inaandaa chapisho ambalo litatolewa Machi mwakani ambalo litakuwa likionyesha idadi kamili ya watanzania.

"Matokeo ya mwanzo yatafuatiwa na taarifa nyingine za kijamii, kiuchumi, kidemografia na mazingira na  machapisho mengine yataendelea kutolewa kadri muda kulingana na ratiba ya utoaji wa matokeo ya sensa," amesema.

Ameongeza kuwa wanaendelea kuandaa chapisho ambalo litatoka Disemba mwaka huu litakuwa likionyesha mgawanyo wa watu wote nchini kiumri kwa ngazi zote.

"Chapisho litaonesha vijana wako wangapi kwa sera ya nchi ya vijana, idadi ya watoto na wazee. lazima litoke Disemba mwaka huu na baada ya hili ndio tutaoa chapisho ambalo litaonesha watanzania wapo wanagapi," amesema.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar Balozi Mohmed Hajj Hamza amesema katika uchambuzi wa matokeo ya mwanzo uwiano wa watu kijinsia kwa Tanzania bara na Visiwani  ni wanaume 95 kwa kila wanawake 100 huku mikoa ya Manyara na Kusini unguja ikionyesha kuwa na idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake.

Ameeleza kuwa  Mikoa hiyo imesababishwa na uhamaji wa wanawake kwenda mikoa mbalimbali kwa ajili ya kujitafutia kipato kwa ajili ya kumudu maisha yao.

“Kusini unguja ambako shughuli kuu ni utalii inawezekana ndio chanzo cha kuwa na wanaume wengi zaidi kuliko wanawake haya ni mawazo ambayo yanahitaji kufanya utafiti wa kina utakao bainisha sababu kwa ajili ya kuweka mipango sahihi kwa wananchi wa maeneo husika,”amesema

Katika hatua nyingine Balozi Hamza alisema ongezeko la idadi ya watu nchiNI  kutoka mwaka 2012 hadi 2022 ni wastani wa asilimia 3.2 kwa mwaka huku akisema taarifa zinazosambazwa mitandaoni zinaonyesha wastani wa ongezeko la idadi ya watu ni asilimia 3.7 zipuuzwe na sio sahihi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU