BRELA, ARIPO WAWATEMBELEA MAWAKALA


 

Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA),Novemba 10, 2022 wakiwa na Mawakala kutoka Kampuni sita (6) za jijini Dar es Salaam, zinazotoa usaidizi wa Usajili wa Alama ya Biashara na Huduma  pamoja na utoaji wa Hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi nchini.

Na Mwandishi wetu

MAAFISA  Waandamizi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kwa kushirikiana na Maafisa Waandamizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), leo tarehe 10 Novemba, 2022  wamefanya ziara ya kutembelea Mawakala sita (6) wa Tanzania waliopo jijini Dar es Salaam, kuona namna ambavyo  wanasajili alama za biashara, huduma pamoja na kutoa  hataza kwa wafanyabiashara na wavumbuzi wa Tanzania kupitia mfumo unaosimamiwa  na ARIPO na kusikiliza changamoto wanazopitia Mawakala hao pindi wanaposajili kupitia mfumo. BRELA inaendelea kuhamasisha wafanyabiashara kusajili Alama za Biashara na Huduma pamoja na kupata Hataza ili kupewe ulinzi wa Kisheria. Mawakala waliotembelewa ni  Bowmans Tanzania, AKP Laws Advocates, FB Attorneys, NexLaw, Lexglobe IP Services na Crystal Associates.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI