BRELA YAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KWENYE MKUTANO MKUU WA 46 WA ARIPO

 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa(wa pili kushoto),  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Bi. Mariam Jecha(kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkugenzi wa Miliki Ubunifu (BRELA) Bw. Seka Kasera (kushoto) na Mwakilishi wa ofisi ya Hakimiliki Tanzania Bw. Philemon Kilaka ( wa pili kulia) mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika Miliki Bunifu kanda ya Afrika(ARIPO) unaofanyika kwa siku tano Maputo, Msumbiji.



Washiriki wa Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo mapema leo tarehe 21 Novemba, 2022 Maputo, Msumbiji.

Na Mwandishi wetu, Maputo

TANZANIA inashiriki katika Mkutano wa 46 wa Baraza la Uongozi la Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), kujadili taarifa mbalimbali za utendaji kazi wa ARIPO  na kupitia taarifa mbalimbali za Itifaki zinazosimamiwa na ARIPO.

Mkutano huo  ulioanza  Novemba 21, 2022 Maputo, Msumbiji, unahudhuriwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, Afisa,  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Bi. Mariam Jecha Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu Bw. Seka Kasera pamoja na mwakilishi kutoka ofisi ya  Hakimiliki Tanzania  Bw. Philimon Kilaka.

BRELA kama Ofisi ya MIliki Ubunifu nchini imekuwa mshiriki mkubwa wa  ARIPO kwenye masuala mbalimbali yanayohusu Miliki Ubunifu kwenye Ukanda wa Afrika. Katika Mkutano huo masuala mbalimbali yatajadiliwa hasa kuhusu Hataza, Maumbo Bunifu, Alama za Biashara na Huduma, Hakimiliki na linzi zingine za Miliki Ubunifu.

Wadau mbalimbali wa ARIPO ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda wameshiriki kwenye ufunguzi wa mkutano. Kwa upande wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) limewakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Bw. Daren Tang.

Mkutano huo wa siku tano utakaohitimishwa tarehe 25 Novemba, 2022 umefunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Msumbiji,  Mhe. Silvino Mareno.

Nchi wanachama 22 wa ARIPO  zinashiriki ikiwa ni pamoja na WIPO  na mashirika mengine ya kikanda na kimataifa


Post a Comment

0 Comments

 MAGARI 25 YA TUME YA MADINI YAMEZINDULIWA,YATASAMBAZWA KWENYE OFISI ZA MAAFISA MADINI