NAPE: WIZARA YA HABARI IMETEKELEZA MAMBO MAKUBWA KWA MUDA MFUPI


 NA Asha  Mwakyonde, Dodooma

WAZIRI wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nauye amesema katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwa wizara hiyo imeweza kutekekeleza mambo makubwa kwa ufanisi yanayoacha alama ikiwemo anuani za makazi.

Nape alitoa kauli hiyo jijini hapa wakati akifungua mafunzo kuhusu miradi inayitekelezwa na wizara yaliyotolewa kwa wadau kikao kikichoshirikisha watumiashi wizara hiyo.

Alisema jambo hilo limefanikiwa kutokana na upendo, umoja na mshikamano wanaoendelea kuuonyesha watumishi hao katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Kujituma kwenu, kupendana, kushirikiana na kuwa na umoja ndio chachu ya mafanikio ya wizara yetu, bado nasisitiza kila alitepewa dhamana ahakikishe anatenda haki kwa anaowaongoza, nawasiii muendelee na umoja huo akikuleta ufanisi na mafanikio zaidi,"alisema.

Akizungumza kuhusu watumishi waliostaafu na kuagwa rasmi katika hafla hiyo, alisema anaaminj kutokana na utendaji wao ukiotukuka mpaka kutunukiwa, baada ya kustaafu, watumishi wengine waliopewa dhama na bado wapo kazini wanayo mengi ya kujifunza kutoka kwao.

"Hapa pia naamini ninyi uliomaliza muda wenu wa utumishi katika wizara hii mmeacha alama, hivyo kila mmoja achukue nafasi hii kutafakari kwa lengo la kuboresha utumishi wake ili akiondoka naye aache alama,"alisema

Aliwapongeza viongozi wa wizara hiyo kwa kutekeleza maagizo yake kwani uendeshaji wa mafunzo hayo na kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vyema na sehemu ya maelekezo aliyoyatoa kwa wizara hiyo.

Nape pia aliipongeza timu ya wizara Kwa kushiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) na kutwaa kombe katika mchezo wa draft upande wa wanawake na kurusha Tufe ambapo timu shiriki za wizara zilikuwa za Shirika la utangazaji TBC, ofisi ya magazeti ya Serikali TSN na Wizara.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI