WAANDISHI WA HABARI WAJENGEWA UWEZO KURIPOTI HABARI ZA CHANJO YA UVIKO-19


 Afisa Afya kutoka Ofisi ya jiji la Dodoma Thobias Kigwinya akizungumzia chanjo ya UVIKO-19 wakati wa kuwajengea uelewa,uwezo Waandishi wa habari  kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo ya namna ya kuandika habari zinazohusu chanjo ya UVIKO-19.

Na Asha Mwakyonde, Dodooma

WATANZANIA wametakiwa kuendelea kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuchanja chanjo na kunawa pamoja na kutumia vitakasa mikono  kwa kuwa chanjo ni salama  na haina madhara yoyote.

Akizungumza na waandishi wa  habari juzi jiijini hapa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uelewa,uwezo waandishi hao  juu ya  kuandika habari za  masula  ya chanjo ya UVIKO-19, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Internews  kupitia Mradi wa Boresha  Habari,Afisa Afya kutoka Ofisi ya jiji la Dodoma  Thobias Kigwinya  amesema haimaanishi mtu akichanga chanjo hiyo hatapata ugonjwa huo  bali unapunguza madhara.

Afisa huyo amesema kuwa mbali na kuchanja chanjo hiyo wananchi wanapaswa kuepuka mikisanyiko isiyo ya lazima huku akieleza kwamba  akipatikana mgonjwa mmoja wa UVIKO-19  inahesabiwa kuwa ni mlipoko tofauti na ilivyo kwa ugonjwa wa ukimwi.

Amesema ugonjwa huo kujitokeza huchukua muda wa siku tatu hadi 14,  hivyo chanjo aina  ya Johnson & Johnson(J&J), huchanjwa Mara moja na  Pfizer, Sinopham, Sinovac na malerna huchomwa mara mbili ili kukamilisha dozi.

Kigwinya ameeleza kuwa  wanahabari wana mchango mkubwa  kuelimisha jamii katika uhamasishaji wa kujikinga na magonjwa  ya mlipuko na umuhimu  wa chanjo  ya UVIKO-19 hivyo ni wajibu kwa kila mwanahabari kuandika habari zenye usahihi na zisizokuwa na mkanganyiko kwa jamii juu ya magonjwa ya mlipuko.

"Waandishi wa habari ni watu muhimu sana katika kuisambaza habari kuwafikia wananchi hivyo mnatakiwa muwe na ufahamu ambao ni mzuri ili unaporipoti habari ya chanjo ya UVIKO-19 uwe unajua unachokiripoti kwa wananchi hawa," amesema.

Amesema ikumbukwe Virusi vipo vingi hujibadilisha kulingana na muda  na mahali husika.

Naye  Mjumbe wa Bodi ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC),Mussa Yusufu akizungumzia maadili ya uandishi  wa  habari kuripoti habari za chanjo amesema  ni vema mwandishi kabla ya kuandika habara afahamu hadhira yake inataka nini. 

Amesema mwandishi anaporipoti habari inayohusu chanjo ya UVIKO-19  asiwe na mihemko binafisi  bali aangalie katika uchaguzi wa vyanzo sahihi, takwimu  muhimu kwa kuangalia  idadi ya watu waliochanjwa aina ya chanjo na ufanisi wa chanjo hiyo.

"Mwandishi anapaswa kutumia lugha sahihi na rahisi katika kuhabarisha Umma. Hii itasaidia kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi kwa jamii," amesema Mjumbe huyo wa UTPC.

Akizungumzia usiri katika kukusanya habari amesema mwandishi wa habari anaweza kupata taarifa kutoka vyanzo mbalimbali miongoni mwa vyanzo hivyo ni waauguzi, Wataalamu wa chanjo,watoa taarifa serikalini na mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa UVIKO-19 huku akisema mtoa taarifa ataandikwa jina endapo ameridhia.

Kwa upande wao waandishi wa habari wahamasishaji wa chanjo ya Uviko-19 mkoa wa Dodoma Bilson Vedastus na Bahati Msanjila  wamewataka Waandishi kutumia vyanzo sahihi wanapohitaji kuandika habari zinazohusu chanjo hiyo na maadili yao.




Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI