MCHUNGAJI KINYAU AITAKA JAMII KUBADILI FIKRA KWA WENYE VVU


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Marco Kinyau akizungumza na baadhi ya waangangalizi  wa Makao ya kukelea watoto yatima na wasiojiweza  Kijiji cha Matumaini. 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa  la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Marco Kinyau ameitaka jamii kubadili fikra ya kuwaona walioambukizwa Virusi vya Ukimwi (VVU), na kudhani kwamba maisha yao yanaishia hapo wakati bado yanaendelea na badala yake wawape upendo wa dhati.

Pia Mchungaji huyo amesema kuwa ni dhambi kwa  mtu mwenye Virusi vya VVU kumuambukiza mwingine kwa makusudi na kumsikitisha  hivyo anapaswa kuwajibika mbele za Mungu kwa kosa hilo.

Mchungaji Kiongozi Kinyau ameyasema hayo Disemba 26, 2022 jijini Dodoma wakati walipowatemblea na kutoa zawadi watoto wanaoishi katika Makao ya watoto yatima na wasiojiweza  Kijiji cha Matumaini, ameeleza kuwa lengo la kwenda  kwenye Makao hayo ni kupeleka upendo kwa watoto hao wanaolelewa hapo kwani wanahitaji upendo huo  kutoka kwa watu wengine tofauti na wanao walea.

Amesema watoto wengi ni yatima na hawana msaada kwa mtu yoyote na kwamba kituo hicho kimechukua jukumu la kuwalea ikiwa ni pamoja na kuwatibu pindi wanapougua.

Mchungaji Kinyau amevitaja vitu walivyopeleka kuwa ni mchele, sukari,unga wa sembe, juice, pipi na biskuti pamoja na kiasi cha fedha.

"Tumeleta hivi vitu  ili watoto washiriki sikukuu ya Krismasi kama wengine wanavyoshiriki na tumepanga siku ya leo kwa kuwa ni siku ya kufungua zawadi ya watu wanaopeana zawadi," amesema Mchungaji.


Aidha ameongeza kuwa sio vizuri kuwatelekeza watoto wakaanza kuitwa watoto wa mitaani ni lazima watakuwa na ndugu wa karibu na kwamba  ni ajabu kuuona mtoto akiwa mtaani wakati ndugu wapo.

Pia amewataka wazazi wasiwatelekeze watoto na badala yake waone ni wajibu wao kuwahudumia hata kwa wale waliofanya maombi ya kuwapeleka kulelewa katika vituo vya kulelea watoto.

Kwa upande wake mmoja wa waangalizi wa watoto  wanaolelewa katika Makao hayo, Sister Christina Shulagi ambaye pia ni muungizi  ameushukuru uongozi wa kanisa hilo la KKKT Dodoma kwa ujio wao wa kuwapa matumaini watoto hao.

"Hii inaonesha wapo watu wengine wanawapenda zaidi hawapo peke yao hata wao wamefurahi kuona ugeni kama huu, kwa niaba ya uongozi wetu nasema ahsante kwa ukarimu wenu, matoleo yenu na kwa upendo ambao mmetuonesha," amesema.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU