MJANE AOMBA MSAADA WA CHAKULA KWA SERIKALI NA WADAU


 Aliyembeba mtoto ni mwandishi wa Habari hizi.

Na Asha Mwakyonde,Chemba

MKAZI wa kijiji cha Daki kilichopo Kata ya Mondo Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma Mwajuma Mwenda (67), ameiomba serikali,mashirika,taasisi na wadau mbalimbali kumsaidia kwa kuwa ni mjane na anawalea wajukuu wake wanne pamoja na mama yao mwenye tatizo la akili.

Akizungumza kijijini hapo hivi karibuni  na mwandishi wa habari hizi  mjane huyo amesema kuwa hana mtu wa kumsaidia mahitaji muhimu ya kijamii  ikiwa ni pampja na huku akiiomba serikali na wadau kumsaidia.

Mjane huyo ameeleza kuwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi alivyolima hakufanikiwa kupata hata debe la mahindi, mtama hivyo hana chakula na kwamba hana uwezo wa fedha kwa ajili ya kununua chakula.

"Ninamwanangu wa kike anatatizo la afya ya akili anawatoto wanne,wa kwanza na wapili nao wanatatizo hilo hilo la mama yao lakini watatu na wanne hawa hawana tatizo," amesema Mwajuma.

Ameongeza kuwa mtoto wake Shufaa Omary (35), wanaume aliozaa nao hawamasaidii hivyo familia yote anaihudumia mwenyewe kwa kufanya vibarua kwa watu.

"Huyu mjukuu wangu unavyomuona ana soma sare za shule zimechakaa  nashindwa kumnunulia sina  uwezo muda mwingine anaenda shuleni bila kuzifua na hapaki mafuta hivyo naombeni Watanzania wenye kuguswa wanisaidie kupitia namba ya simu 0752881583," amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bunge Tesa amesema kuwa kama ikitokea taasisi,Shirika linatoa msaada wangemfanyia utaratibu wa kuweza kumsaidia.

"Hata Mpango  wa kunusuru kaya maskini (Tasaf), angekuwepo tungemuingiza lakini aliolewa hivyo hivyo alivyo, kwa sasa tayari tumeshamwandikisha tunasubiri serikali kupitia Tasaf ianze utekelezaji wake," amesema Tesa.


Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU