VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA, DINI WAMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA POLISI ILI KUIMARISHA ULINZI.


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma

JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa limejipanga vizuri kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuzingatia nidhamu,haki,weledi na uadilifu na kwamba hali ya ulinzi na usalama wa nchi katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2022 na mwanzoni mwa mwaka 2023 umeimarika kwa asilimia kubwa ni shwari kwani uhalifu mkubwa umedhibitiwa.

Pia Jesho hilo limetoa wito kwa viongozi wa serikali za Mitaa waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi Kata,Shehia kuanzisha na kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi ili visaidie kufanya doria katika mitaa na kuwanyima wahalifu fursa ya kutenda uhalifu.

Akizungumza jijini hapa leo Disemba 22,2022,Msemaji wa Jeshi hilo,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP),David Misime  amewaomba viongozi wa dini kuhimiza na kuendelea kutoa fundisho kwa waumini wao, kufungua na kuimarisha kamati za usalama katika nyumba za ibada  na kufanya vikao na Polisi kwa lengo la kuweka mikakati na mbinu za namna ya kuimarisha ulinzi wakati wa sikukuu za misho na mwanza wa mwaka.

"Wazazi,walezi tunawataka kuwalinda watoto ili wasijiingize kwenye vitendo vya uhalifu au kutendewa kitendo chochote cha kihalifu hivyo kila mmoja wetu ahakikishe popote pale atakapokwenda mtoto hasa maeneo ya mikusanyiko ya burudani kama fukwe aambatane na mtu mzima,"amesema.

Akizungumzia ajali za barabarani Msemaji huyo amesema kuwa Jeshi la Polisi linatoa wito kwa kila mtumia barabara kuondokana na tamaduni za kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani pale tu anapomwona askari polisi na kwamba huo ni utamaduni unaowasababishia ajali na hazitakiwi kuendelea.

"Utafiti umeonesha katika ajali zilitotokea asilimia 75 zimesababishwa na uzembe wetu binadamu hasa wa kutokufuata sheria na kanuni kwa baadhi ya watumia barabara hadi amuone askari polisi," Ameongeza.

Uzembe huu wa kibinadamu uliobainika ni pamoja na kuendesha chombo cha moto kwa mwendo kasi, kuendelea ukiwa umetumia kilevi  mfano utafiti tulioufanya kuelekea sikukuu hizi za mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka umebaini baadhi ya madereva kuwa na pombe kwenye magari na kuendelea kunywa wakati wanaendesha gari," amesema SACP Misime.

Amefafanua kuwa kuna baadhi ya madereva wanaposimama kupata chakula hunywa pombe wakati wanafahamu bado wanaendelea na safari.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU