WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA MAELEKEZO KWA WIZARA YA MIFUGO


Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka  Wizara ya Mifugo na Uvuvi   kushirikiana na wadau, wafugaji kuhakikisha  wanashiriki kikamilifu katika kuhamasisha mabadiliko ya mfumo wa ufugaji ikiwa ni pamoja  ufugaji wa kukaa katika eneo moja bila kuhamahama iwe wafugaji hao waweze kulima malisho badala ya kutegemea malisho ya asili.

Pia Waziri Mkuu ameielekeza Wizara hiyo  na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya tathmini ya maeneo ya ufugaji yaliyopo katika maeneo yao nikiwa ni pamoja na kuangalia kiasi cha mifugo kinachoweza kufugwa na kama  mifugo hiyo itazidi uwezo wa eneo husika, wafugaji waelekezwe kuvuna mifugo yao.

Waziri Mkuu Majaliwa  ametoa maelekezo hayo jijini hapa Disemba 19,2022 wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau wa Sekta ya Mifugo
 wenye kauli mbiu isemayo “Mwelekeo Mpya wa Sekta ya Mifugo Nchini amesema wafugaji wahamasishwe kuvuna mifugo yao ili kuwawezesha kupata bei nzuri sokoni.

Amesema  hiyo itasaidia kupunguza changamoto za malisho hususan wakati wa ukame na kwamba uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za mifugo uimarishwe Kwa lengo la kuongeza tija katika sekta ya mifugo pamoja na kuwahamasisha wafugaji kutumia mifugo bora ambayo imefanyiwa utafiti wa kina zaidi.


"Kasi ya uvunaji wa mifugo hapa  nchini ni  asilimia 10 ikilinganishwa na viwango bora vya uvunaji wa mifugo kitaifa ambavyo ni kati ya asilimia 20 na 25 hii inaonesha bado ipo chini hivyo viongozi na watendaji wa Serikali, hakikisheni mnashirikiana na wadau hasa hawa wafugaji katika kuwekeza na kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo majosho, malambo, visima vya maji na maeneo ya malisho," ameeleza.

Pia, ameelekeza wizara hiyo kuimarisha huduma za ugani kwenye sekta ya mifugo kwa kuweka vigezo vya kupima utendaji kazi na kuwafuatilia Wagani wote nchini ikiwa ni pamoja na kuhimiza matumizi ya TEHAMA, kuendelea kuwapatia vyombo vya usafiri na mafunzo rejea kuhusu teknolojia mpya za ufugaji wenye tija na wa kibiashara.

Aidha, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi ishirikiane na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kutatua migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi. 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  anatamani kuona sekta hii inaleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kukuza zaidi pato la wananchi hasa katika kutoa ajira bila kuathiri mazingira na maendeleo ya sekta nyingine.

Awali, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki Sekta ya Mifugo inakabiliwa na changamoto mbalimbali, na kwamba watatumia mkutano huo kujadili namna ya ufugaji bora pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. 

"Lengo la mkutano huu ni pamoja na kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya mifugo Ili kujadili kwa kina kuhusu mwelekeo mpya wa sekta ya hii nchini sambamba  na kuwajengea uwezo wafugaji ili wafuge kwa tija na kibiashara kama wawekezaji kwenye sekta ya mifugo.

Kwa upande wake Mfugaji Molell Saitoto amesema kuwa mkutano huo unatoa dira njema kwa wafugaji na kwamba baada ya kumtano wataenda kuwaelimisha wenzao namna ya kukaa sehemu moja bila kuhamahama.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI