WIZARA YA MIFUGO YAKANUSHA ZUIO LA WAVUVI WA DAGAA

Na Asha Mwakyonde, Dodooma

SERIKALI kupitia wizara ya Mifugo na Uvuvi imekanusha zuio la wavuvi wa Dagaa katika Ziwa Victoria kuacha matumizi ya Taa za Umeme wa Jua (Sola) zinazotumia Betri za Pikipiki kuanzia Januari Mosi 2023 huku ikiwataka wavuvi hao kuendelea na shughuli zao kwa kutumia zana na njia rafiki zinazolinda rasilimali za Uvuvi.

Kanusho la Serikali limetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Uvuvi wizara ya Mifugo na Uvuvi Magese Bulayi ambapo ameeleza kuwa agizo la ukomo wa matumizi ya taa hizo ni madai yasiyo na ukweli wowote hivyo wavuvi wa dagaa katika ziwa Victoria wanapaswa kupuuza na kuendelea na majukumu yao.

Mkurugenzi huyo akizungumzia kuhusu athari za matumizi ya Taa hizo zinazotumia Betri za pikipiki  amesema tayari serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania TAFIRI ilifanya Utafiti na kutoa mapendekezo ya aina ya Taa zinazokubalika katika Uvuvi ikiwamo za aina hiyo pamoja na zinazotumia mafuta ya taa (Karabai).

Ameongeza kuwa Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi nchini unazingatia sera ya Taifa ya Uvuvi ya Mwaka 2015, Sheria ya Uvuvi na 22 ya mwaka 2003 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2009, na marekebisho ya mwaka 2018,2019,2020 na 2022 Huku Uvuvi wa Dagaa ukiwa chini ya kanuni ya 66 ya kanuni za mwaka 2009 na marekebisho yake kuhusu matumizi ya Taa za Sola

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI