CHONGOLO AWAONYA VIONGOZI WANAOWALALAMIKIA WATENDAJI WALIO CHINI YAO


 Na Asha Mwakyonde,Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amewaonya viongozi wanaolalamika kuhusu maeneo wanayopewa kufanyia kazi hali ambayo inawavunja moyo wananchi ambao wanawategemea kutatuliwa kero zao.

Pia amesema anashangaa kuona baadhi ya viongozi wakiwemo Mawaziri,wakuu wa mikoa na baadhi ya viongozi wanalalamika kutopewa ushirikiano na watumishi hali ambayo imekistua chama na kuwatathimini kwamba majukumu waliyopewa hawayawezi na kuwataka wajitathmini.

Chongolo ametoa onyo hilo jijini Dodoma leo Januari 24,2023,  wakati wakupokelewa kwa Wajumbe wa Secretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi Taifa ambapo amesema hawatakuwa na huruma katika kuchukua hatua kali za kisheria kwa kuwawajibisha wahusika.

Katibu huyo amewatangazia kiama viongozi wanaotumia muda mwingi kulalamika na kwamba kulalamika kwao kunaonesha wazi kuwa hawatoshi katika nafasi walizoteuliwa au kuchaguliwa.

"Ni aibu mfano unawakuta watumishi wa serikali wanaenda kwenye vyomba vya habari wanawalalamikia watendaji waliopo chini yao kuwa hawasaidii kufanya kazi kwa kitendo hiki kinaonesha wazi kuwa hautoshi ni sawa na katibu mkuu kuwalalamikia waliopo chini yake kuwa hawasaidii kazi, unawezaje wakati unatakiwa kutumia mamlaka uliyo nayo?,”amehoji Chongolo.

Pia Chongolo ameeleza kuwa Sekretarieti hiyo imeaminiwa zaidi Lengo likiwa ni kuhakikisha inafanya kazi kwa nia na kutatua matatizo ya watanzania na kujibu hoja.

Akizungumzia suala la kushika dola Katibu huyo amesema Chama chochote cha siasa kina kazi moja ya kutafuta na kushika na kuisimamia dola na kwamba kazi yao kwa sasa ni kuisimamia dola hiyo.

"Tuna kazi ya kusimamaia dola tuliyopewa na dhamana ya kuishika na wananchi ili ifikapo mwaka 2024 na 2025 tusiende kuulizwa na wananchi. Ndugu zangu 2019 chama kilipewa dhamani ya kushika nafasi za serikali za mitaa wajibu huo unatakiwa kusimamaia ili yaendeleee kuaminiwa zaidi na zaidi," ameeleza.

“Changamoto nyingine tulitonayo kwa baadhi yetu ni baadhi ya watumishi waliopewa majukumu lakini lakini hawajui majukumu ya nafasi tulizopewa ,mkuu w mkoa badala ya kutimiza wajibu wake anakaa analalamika hatupo kwenye wajibu wa kusikiliza malalamiko yuko kwenye ajibu wa kutenda kama waxiri umepewa dhamana ya kutjmikia unashindwa kutumikia unachelewesha kutimiza malengo huo ndio wajibu tunaonenda kuufanya na tutaufnaya kwelimwkweli.

“Wananchi wanataka miungdo mbinu wananchi wanataka dawa za mifugo wannchi wanataka huduma sio maneneo,kama ni wachimbaji wadogo na wakubwa watendedewe haki sawasawa kama ni wakandarasi wa ndani na nje watendewe sawasawa wasipotendewa sawasawa watatuonyoshea kidole tukiruhusu wananchi watunyooshee vidole tutakua hatutendi sawasawa”ameeleza Chongolo.

“Mimi ni chongolo ila nikiwa hapa mimi ni Katibu Mkuu wa chama cha mapinduzi hivyo sitaki kuona viongozi watakaosababisha maswali mengi kwa watanzania yasiyokuwa na majibu ntunataka vitendo siyo maneneo,”amesema.

Katika hatua nyingine Chongolo amesema kuwa Wiki hii wanaanza ziara mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kukagua miradi kuanzia ngazi ya shina huku akiwataka watendaji wa juu wakihakikisha wanatoa ushirikiano na watumishi wa ngazi ya chini.

Aidha Chongolo amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya kuchekeana na kufimbiana macho katika mambo ya msingi ambayo yanagusa maisha ya watu.

Kwa upande wake Katibu wa itikadi na uenezi wa hicho ,Sophia Mjema amesema kuwa kwa nafasi aliyopewa anaenda kufanyakazi kwa mitazamo tofauti kwani kabla ya kwenda kwa wananchi lazima idara hiyo uelimishaji uwe sawa .

“Lazima mabalozi wetu wakajue wananchi wanataka nini lazima ndugu zetu tutakapokwenda kwa wananchi tutaenda mpaka ngazi za vitongoji tukajue wananchi wanataka nini,”amesema Mjema.

Amesema katika kukitangaza chama wana CCM wanatakiwa kufanyakazi wote kwa pamoja kwani hakuna mwingine atakae kilinda chama bali ni wao.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI