WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAPATA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA KWA KUTOA HUDUMA KWA UPANDE WA WIZARA

📍Yatoa huduma za sheria kwa wananchi zaidi ya 2,000 Sabasaba

Na Asha Mwakyonde, DAR ES SALAAM

WIZARA ya Katiba na Sheria imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la wizara, mafanikio yanayoakisi namna ilivyoshiriki kikamilifu katika kutoa huduma mbalimbali za kisheria kwa wananchi. Huduma hizo zilijumuisha ushauri kuhusu mirathi, ndoa, masuala ya ardhi pamoja na uandaaji wa nyaraka mbalimbali za kisheria.

Pia Wizara hiyo imefanikiwa kuwahudumia wananchi zaidi ya 2,800 kupitia utoaji wa huduma za msaada wa kisheria katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF),'Sabasaba'  hatua inayoonesha mwitikio mkubwa wa wananchi katika kutafuta haki na ushauri wa kisheria.

Akizungumza leo Julai 13,2026
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Utatuzi wa Migogoro kutoka Wizara hiyo  Felix Chakila amesema huduma zilizotolewa zimekuwa sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wanapata haki na ushauri wa kisheria kwa urahisi.



Amesema ingawa wananchi hawakulipia huduma hizo, Serikali ndiyo iliyogharamia utoaji wake ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata msaada wa kisheria na suluhisho la changamoto mbalimbali zinazowakabili.

"Tumefanikiwa kuwahudumia wananchi takribani 2,800. Hii ni sehemu ya kurejesha kwa jamii na kutekeleza wajibu wetu kama Wizara na Serikali wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za sheria kwa ukaribu na kwa ufanisi," amesema Chakila.

Amebainisha kuwa mwitikio mkubwa uliojitokeza katika banda la Wizara unaonesha bado kuna uhitaji mkubwa wa huduma za msaada wa kisheria, jambo linaloipa Serikali wajibu wa kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma hizo kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya sheria.

Chakila ameeleza kutokana na muda mfupi wa maonesho, si wananchi wote waliofika waliweza kuhudumiwa, na kwamba uzoefu huo umeonesha umuhimu wa kuongeza wigo wa utoaji wa huduma hizo katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia huduma zinazotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na wadau wa haki ili kupata ushauri na utatuzi wa migogoro kwa njia zinazozingatia sheria.

Amesisitiza kuwa Wizara itaende
lea kushirikiana na taasisi mbalimbali za haki ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuhakikisha huduma za kisheria zinapatikana kwa urahisi, zikiwasaidia kulinda haki zao na kutatua migogoro kwa wakati.

Post a Comment

0 Comments

SERIKALI IMETENGA BILIONI 1 UKARABATI MAKAZI YA WAZEE NCHINI - NAIBU WAZIRI MAHUNDI