Na Asha Mwakyonde,Dodoma
MAMLAKA ya kupambana na Kudhibiti Dawa za kulevya Nchini (DCEA), imesema kuwa imejipanga kudhibiti mipaka ya wazi ikiwemo mipaka ya baharini ambayo imeonekana kuwa changamoto kubwa inayochangia uingizwaji na utolewaji wa dawa hizo.
Akizungumza Jijini Dodoma katika banda la Mamlaka hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Square, kutoka DCEA Dk. Christian Mbwasi amesema maeneo ya bahari yamekuwa changamoto kutokana na Tanzania kuwa na eneo huru na la wazi la ukanda wa bahari ambalo vyombo vya ulinzi na usalama vinashindwa kuyafikia kwa wakati mmoja kutokana na maeneo hayo kuwa makubwa.
Dk. Mbwasi amesema kuwa licha ya changamoto hiyo Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo , kutoe Elimu Kwa umma kuhusu madhara ya dawa hizo, kuwajengea uwezo watendaji kujua Nini tatizo kwenye jamii , pamoja na kuongeza mashirikiano na mlaka nyingine za ulinzi.
Hata hivyo Dkt, Christian ameiomba jamiia kutoa ushirikiano kwa kutoa Taarifa kama kunauhalifu wa dawa za kulevya unaendelea kwenye maeneo yao huku akisiaitiza kuwa mtu yeyote atakae toa Taarifa juu ya vukundi au watu wanaojihusisha na Dawa za kulevya atakuwa salama.
Dhima ya Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya ni kudhibiti na Kupambana na Biashara haramu ya dawa hizo na matumizi yake kupitia mikakati ya kisekta Kwa ajili ya ustawi wa Taifa
0 Comments