MAMA NA BABA LISHE WA MACHINJIO YA VINGUNGUTI WAMKABIDHI ZAWADI YA MBUZI MSTAHIKI MEYA KUMBILAMOTO

Na Asha Mwakyonde, Dar es salaam

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto amekabidhiwa zawadi ya mbuzi na Wafanyabiashara wadogo wadogo  wa chakula Mama na baba lishe wa eneo la Machinjio ya Vingunguti ikiwa ni ishara ya upando Kwa yale anayowatendea Wafanyabiashara hao.

Akizungumzia furaha yake Mstahiki Meya Kumbilamoto jijini Dar es salaam Januari 13,2023 amewataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu kwani kwa sasa wanamalizia kujenge jengo la wauza utumbo.

Mstahiki  Meya huyo amesema kuwa kunapotokea soko litakapojengwa kuna watu wapya huwa wanajichomeka ambapo mtendaji wa serikali ya mtaa mtendaji wa mtaa pampja na wajumbe wa serikali ya mtaa mchukue takwimu za wafanyabiasha ambao wapo kwenye eneo hili baada ya ukarabati ili warudi katika nafasi zao.

" Nakushukuru mtendaji  makubaliano yetu ya kuwapanga pamoja na watu wanunue  miamvuli yamekamilika, hata mgeni akija anakuta kupo safi. 
Wakati naongea na simu nilikuwa naongea na Mhandisi wa jiji kuhusu mchakato  wa usanifu umefikia wapi ameniambia tayari wameshafanya usanifu  wa kina na faili limeshafika kwa Mkurugenzi," ameeleza.


Ameongeza kuwa wanachotaka ni kuona kwamba watu wa masaki na oysterbay na Upanga  wakisem wanakuja kula chakula cha mchana katika soko la vingunguti nyama inapopatikana wakute maeneo mazingira na safi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao Mohamed mwekwa  maarufu Mwarabu pool, amesema wamempatia Meya huyo zawadi ya mbuzi kutokana na juhudi zake anazozifanya kwa wafanyabiashara hao ikiwa ni pamoja na kuwapatia elimu ya Mazingira na ajira kwa vijana.

"Tuliona ni jambo la heri kumpatia zawadi Meya ni mtu mkubwa lakini kwa namna anavyowapatia sapoti wafanyabiashara hawa wameona nao wampatie zawadi hii," amesema Mwarabu Pool.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU