KAMATI YA USHAURI HALMASHAURI YA MJI MASASI (DCC) YAKUTANA KUISHAURI SERIKALI


Na Mwandishi wetu,Masasi

KAMATI ya Ushauri Halmashauri ya Mji Masasi (DCC) January 20,2023 Imekutana katika kikao maalum cha kushauri Rasmu ya Bajeti ya Halmashauri ya Mji Masasi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akiongoza kikao hicho katika Mji wa Masasi leo Januari 20,2023 Mwenyekiti wa DCC ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Mariamu Chaurembo kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Masasi, amewaomba wajumbe kuishauri serikali kwa busara huku akisema kuwa ushauri wa wajumbe hao kuwa ni tija kwa maendeleo ya Wilaya hiyo.

Naye afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Masasi Wilfred Lazaro amesema kuwa Rasimu hii ya Bajeti imezingatia Dira ya maendeleo ya Taifa kufikia 2025, Mpango wa tatu wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano (2021/2022-2025-2026).

Pamoja na Mambo mengine Bajeti hiyo imejikita katika kuleta matokeo chanya na yenye kugusa maisha ya Wananchi mmoja mmoja, Pia Bajeti, imejikita katika Miradi inayolenga kuzingatia malengo endelevu ya mwaka 2030.

 Aidha Lazaro ameieleza kamati kuwa Halmashauri inatarajia kutumia Shilingi 24,014,358,000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kati ya hizo Mapato ya ndani ni Shilingi 2,855,980,500 Ruzuku ya Matumizi ya kawaida na mishahara ni Shilingi 13,708,650,000 na Miradi ya Maendeleo ni Shilingi 7,450,978,000. 

Chaurembo amepongeza rasimu ya bajeti kwakuweka vipaumbele vya huduma za kijamii ambazo ni Elimu,Afya,na zinginezo ,pia ameomba utekelezaji wa vipaumbele ufanyiwe kazi kwani kuwa na afya bora ndio mafanikio ya wanamasasi wote.

Wajumbe wa kamati ya ushauri nao wamepata muda mzuri na kushauri maeneo mbalimbali katika Rasmu ya Bajeti,hivyo kikao kimekuwa na mafanikio makubwa zaidi kwani Bajeti inaaksi pia fursa kwa vijana na Wanawake, Rasimu hiyo ushauri wa DCC Utafikishwa kwenye kamati za kudumu za Halmashauri pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Masasi.


Kikao kimehudhuriwa na Viongozi wa Vyama vya siasa, Viongozi wa Sekta binafsi, Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata zote, Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ,Wazee Maarufu,Viongozi, Kaimu Mkurugenzi Jumanne Chaula ambaye ni katibu wa kikao hicho na Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu (DC) ambaye pia ni mwenyekiti wa kikao hichi.

Post a Comment

0 Comments

MAJALIWA: MJI KONDOA TUMEKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 126 KIPINDI CHA JULAI HADI JUNI MWAKA HUU