Na Asha Mwakyonde,Dodoma
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa .Adolf Mkenda amewataka Wakuu wa shule binafisi kuangalia misaada ya vitabu wanavyopatiwa kama maadhui yake yana maadili.
Pia Prof. Mkenda amesema ni kweli utandawazi hasa masuala ya simu yamewezesha taarifa ambazo zinawashawishi watoto kwenda kufanya mambo ambayo ni mabaya na kwamba suala la malezi linaanzia nyumbani ni la mtambuka.
Waziri Mkenda ameyasema hayo leo Januari 21,2023 Jijini Dodoma katika kikao cha Wadau wa Elimu wa Shule binafisi ambacho pia kimehudhiriwa na viongozi wa Idara mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo amesema kama kuna watu wanafanya kampeni na kuona suala hilo lipitie shuleni kwa watoto ni lazima Shule hizo ziwekewe ulinzi.
Prof. Mkenda amesema kuwa dunia nzima hasa nchi za Magharibi hakuna nchi inayoruhusu mambo ya ngono kwa watoto na kuwataka Wakuu wa shule binafisi kuangalia vitabu vyote vimaeandikwa maudhui gani.
"Kama ni kweli kuna watu wanafanya kampeni na kuona hili suala lipitia shuleni kwa watoto wetu ina maana shule zetu lazima ziwe na ulinzi mkubwa sana," amesema Waziri huyo.
Ameongeza kuwa kazi ya ulinzi kwa watoto ni la sekta nyeti na kwamba hakuna kigugumizi katika kulisemea suala hilo.
Prof. Mkenda amebainisha kuwa shule zote za binafisi zina umuhimu mkubwa kwa serikali na kwamba wanathamini mchango wa shule hizo.
Mmoja wa Wadau hao ,Naibu Mkurugenzi wa Elimu kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Khamis Ally amewataka viongozi wa dini wa madhehebu tofauti tofauti ili kutoa y elimu ya madili ,dini kwa wanafunzi.
"Serikali iangalie suala la maadili shuleni kwani Taifa lolote ni maadili lisipokuwa na maadili linakuwa ni la hovyo," amesema Ally.
0 Comments