WANAFUNZI WA VYUO VYA KATI NA VIKUU KUTOA ELIMU YA AFYA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA JAMII

 

Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imesema itaweka mkakati wa kuwatumia wanafunzi wanaosoma kozi za afya vyuo vya kati na vyuo vikuu ili kutoa elimu ya afya katika shule za Msingi ,Sekondari na ngazi ya jamii lengo likiwa ni kuhakikisha elimu hiyo inawafikia.

Akizungumza jijini Dodoma katika Warsha ya siku mbili ya “Afya Day”,iliyoratibiwa na wizara hiyo pamoja na wadau mbalimbali iliyofanyika katika 
 Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Yohane (St.John’s),Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya ELimu ya Afya kwa Umma,Idara ya Kinga wa Wizara ya Afya Dk.Tumaini Haonga amesema kuwa wanafunafunzi hao wananafasi kubwa ya kutoa kueneza elimu kwa haraka.

Dk.Haonga amesema ili kuhakikisha
elimu hiyo inafika kwa wakati wizara imeona ni vema wanafunafunzi hao wakatumika kwa kuwa ni moja ya 

"Wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu wanaosomea kozi za afya wakatumike kutoa elimu ya afya kama sehemu ya mafunzo ya vitendo kwao na itafika kwa wakati shuleni," ameeleza Dk. Haonga.

Ameongeza kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu anayesoma ngazi ya Astashahada,Stashahada na Shahada kwenye eneo la afya muda wa kufanya mazoezi ni muhimu akafanyie shuleni 

Dk. Haonga amesema kuna changamoto nyingi kwa vijana ikiwemo masuala ya lishe,afya uzazi  na kwamba ataelekeza wadau wa maendeleo kuongeza bajeti ili kuwezesha suala hilo liwe la utekelezaji Dodoma na nchi nzima kwa ujumla.

Akizungumzia umuhimu wa vyombo vya habari ,Dk.Haonga amesema waandishi wa Habari wana mchango mkubwa katika eneo la Elimu ya Afya kwa Umma ili kuondoa dhana ya upotoshaji kwa jamii.

 "Tunawahitaji sana waandishi wa habari kwenye eneo la Elimu ya Afya kwa Umma ili waweze kutusaidia kufafanua dhana potofu zinazoibuka kuhusu masuala ya afya zinazoweza kusababisha wananchi wasizingatie kanuni bora za afya.

Afisa Mpango wa Afya shuleni ,Elimu ya Afya kwa Umma ,Idara ya Kinga,Wizara ya Afya,Magdalena Dinawi amesema kwa taratibu za nchi kijana anaweza kupima Virusi vya UKIMWI kuanzia miaka 15 na kuendelea bila ridhaa ya wazazi wake.

Kwa upande wake mwenyekiti wa timu za uhamasishaji uchangiaji damu kanda ya kati Dkt.Leah Kitundya amesema mahitaji ya damu ni makubwa hivyo amehimiza wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia damu.

“Haijawahi tokea damu zikatosha ,unapochangia leo damu zinamaliza muda wa matumizi[Expire]ndani ya siku 35,hivyo siku 35 huwa hazifiki damu zinaisha ,makusanyo ni madogo mahitaji ni makubwa ,kinachotakiwa damu zikusanywe zimsubiri mgonjwa elimu inahitajika sana”amesema.
 
Katika Warsha Warsha hiyo wananchi 138 walijitokeza kuchangia damu ambapo chupa130 zilipatikana  na pia huduma mbalimbali zilitolewa zikiwamo za kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi kwa vijana, upimaji wa Kiwango cha Sukari mwilini, Shinikizo la Damu (BP) na maambukizi ya VVU.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI