TANESCO KUZALISHA MEGAWATI 5000 IFIKAPO 2025

Na Asha Mwakyonde Dodoma 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema kwa sasa lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820 ambapo mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee.

Maendeleo ya ujenzi Bwawa la Mwalimu Nyerere umefikia asislimia 88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma  Februari 22,2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa TANESCO, Martin Mwambenewakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za shirika hilo amesema mkakati wao hadi kufikia mwaka 2025  litakuwa limefikia malengo ya uzalishaji wa Megawati 5000,kutokana na baadhi  ya miradi ambayo inachangia kuongeza uzalishaji wa umeme katika gridi ya taifa kila mwaka.

Mwambene ameeleza kuwa katika mradi wa Grid Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6000,mita 700,000 za umeme, nguzo 380,000,ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa km 40,000, ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takribani kilomita 948 na ujenzi wa vituo 14 vya kupooza umeme. 

"TANESCO kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake,"amesema

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI