TCU: TANZANIA IMELENGA KUWA NA WATU WENYE KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIUCHUMI

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof.Charles Kihampa amesema Tanzania imelenga kuwa Taifa la watu wenye maarifa,ujuzi,weledi na uwezo wa kutatua changamoto za kiuchumi ifikapo mwaka 2025.

Pia amesema TCU imeendelea kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na mifumo ya ndani ya vyuo vikuu ili kuhakikisha vyuo hivyo vinaendana na mwelekeo wa nchi.

Akizungumza jijini Dodoma  Februari 22,2023 wakati akizungumzia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume hiyo  kwa kipindi cha miaka wiwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita amesema lengo kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Prof. Kihampa amesema Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi,wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya Umma na binafsi hapa nchini lengo likiwa ni kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa taasisi zao.

Akizungumzia kuongezeka kwa fursa za masomo ya elimu ya juu na idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu nchini, amesema  program za shahada ya kwanza zimeongezeka kutoka 157,770 mwaka 2020/2021 hadi 172,168 mwaka 2022/2023 ikiwa ni ongezeko la nafasi 14,398 sawa na asilimia 9.1

Pia idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 259,266 mwaka 2020/2021 hadi 295,919 mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 14.1 idadi hii inatarajiwa kuongezeka Kwa mwaka wa masomo 2022/2023

Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) ni taasisi ya Serikali, iliyoundwa mwaka 2005 Kwa Sheria ya vyuo vikuu sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI