Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye moja ya mabanda kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere square Jijini
Na Sifa Lubasi, Dodoma
WANANCHI wametakiwa kuchukua tahadhali wanapotibu majeraha ya moto ili kupunguza uwezekano wa jeraha kuwa kubwa zaidi na kushindwa kutibika kwa wakati na hata kusababisha kifo
Akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yanayofanyika katika viwanja vya Nyerere square,Ofisa Muuguzi Msaidizi Mwandamizi daraja la pili David Mpaguke kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alisema majanga ya moto hutokea popote na wakati wowote
Alisema kuwa ulimwenguni kote kila mwaka takribani watu milioni moja hutafuta matibabu kutokana na kuungua moto.
Alisema kuwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa mwaka 2020 hadi 2022 imepokea na kulaza wagonjwa 225 walioungua mwa moto asilimia 87 walipona na asilimia 13 walikufa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kucheleweshwa kufikishwa hospitali, mika na desturi ya jamii,Imani na changamoto za Uchumi.
Alisema kuwa kitaalam mtu anapoungua amwagie jeraha maji safi ili kupunguza joto lisiathiri ngozi na misuli, Kisha apewe Panadol kwa ajili ya kutuliza maumivu na awahishwe hospitali
"Majeraha madogo ya moto, haraka mwaga maji baridi juu ya ngozi iliyoungua kwa dakika 15 hadi 30 husaidia kupunguza joti lisiathiri ngozi na misuli,"alisema.
Pia alisema kuwa ulaji wa vyakula vingi vyenye virutubishi vikiwemo protini ya ziada vinahitajika kusaidia kidonda cha moto kupona.
"Mgonjwa apatiwe vyakula vya Protini ili Kujenga mwili ili nyama ziwe zinajengwa pia kufanya mazoezi ili kuzuia ulemavu unaoweza kutokea," alisema
Alisema kuwa kama majeraha ya Moto Ni makubwa mgonjwa hufanyiwa upasuaji wa kupandikizwa ngozi.
Alisema kuwa kumekuwa na njia mbalimbali za asili za kutibu majeraha ya Moto lakini nyingi so salama.
"Asali inatibu kidonda lakini si kila kidonda kinahitaji asali , Aina ya vidonda vilivyochimbika Sana husaidia Kujenga misuli lakini asali peke yake sio dawa,"alisema
Pia alisema wengine wakiungua wanamwagia mafuta ya taa, Kuweka chumvi, manyoya ya sungura lakini njia hizo si salama kwani zinaongeza uwezekano wa mgonjwa kupata tetenus, kuongeza uchafu kwenye kidonda .
Alisema kuwa majeraha ya moto yamekuwa yakusababisha vifo kutokana na muda ambao mgojwa aliwahi kwenye matibabu,ukubwa wa majeraha husababisha viungo vingine mwilini kushindwa kufanya kazi.
"Ngozi ikitoka husababisha mtu kupoteza maji mengi sana,wakati mwingine kupelekea figo kushindwa kufanya kazi kwa vile mwili hauna maji," alisema.
Alisema kuwa wagojwa hufanyiwa upasuaji ili kurekbisha japokuwa haurudi kwa asilimia 100 inategemea Moto ulimpa athari kwa kiasi gani ," alisema.
0 Comments