MOI YATOA USHAURI KWA WAKAZI WA DODOOMA


 Na Asha Mwakyonde, Dodoma

KIONGOZI wa Jopo la Wauguzi na Watumishi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI),Elizabeth Mbaga amesema  kundi liliongoza kutembelea banda la taasisi hiyo katika maadhimisho ya miaka 70 ya Baraza la Uuguzi na Ukunga yaliyoenda sambamba na maonesho ambayo yanayofanyika  katika viwanja vya Nyerere square ni wazee.

Akizingumza Jijini Dodoma Machi 18,2023 katika banda hilo Mbaga ameeleza kuwa kundi liloongozo kwa idadi kutembelea banda la MOI ni wazee wanawake na vijana wenye umri kuanzia 35 na kuendelea ambao walikuwa na shida ya magoti na migongo.

Mbaga amesema kuwa waliojitokeza ni wale wenye shida za mbalimbali zikiwamo za mgongo,miguu, na wanaosumbuliwa magoti ambapo huenda kwenye maduka ya dawa na kupatiwa dawa bila kufanya vipimo.

"Tumekuja hapa kwenye baraza hili la wauguzi kuonesha huduma zetu ambazo tunazifanya MOI tupo hapa kuanzia Machi 17 hadi 19, tumeona wananchi wa Dodoma wamejitokeza kwa wingi kwenye maonesho haya na kupata huduma,amesema Mbaga.

Amesema kuwa katika maonesho hayo wametoa huduma ya ushauri kwa wananchi waliojitokeza kuhusu huduma wanazozitoa katika taasisi hiyo pamoja na kuwaonesha kazi wanazozifanya.

"Wapo walifika katika banda hili kwa ajili ya kueleza shida zao,wengine kuja kupata ushauri na wengine wanapoelezewa na wataalam anasema kwamba anatatizo hili ndipo tunapotoa elimu na ushauri" ameeleza Mbaga.

Ameongeza kuwa baada ya ushauri wanaugungulika kuwa wanatatizo wanawashauri kwenda sehemu ikiwa ni pamoja na kumuona daktari ili kuandikiwa vipimo husika kutokana na ugonjwa anaougua

Post a Comment

0 Comments

 KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YANOLEWA