WRRB YAWAONYA MADALALI WANAOWARUBUNI WAKULIMA


 Na Asha Mwakyonde Dodooma

BODI ya Usimamizi wa Stakabadhi ghalani (WRRB),imewataka madalali kuacha kuwarubuni wakulima na badala yake wajiunge katika Mfumo wa Stakabadhi ghalani ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya ushindani iliyopo sokoni.

Akizungumza jijini Dodoma Feburuari 15,2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Asangye Bangu wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya WRRB, amesema wakulima  kuuza mazao shambani inaendelea kuwadidimiza kwa sababu madalali wengi wananunua mazao kwa bei ya chini tofauti na bei iliyopo kwenye mfumo.

Mkurugenzi huyo amesema baadhi ya  madalali wamekuwa wakiwarubuni wakulima kwa kutumia mbinu za kwenda mashambani na kuwadalalia mazao
yao kwa bei ya chini kitu ambacho kinaendelea kudidimiza kinaendeleo.

Ameongeza kuwa kumekuwa na wimbi la watu wanaokwenda mashambani kwa wakulima wenye hali ya chini na kununua mazao kwa bei ya chini jambo ambalo linamdidimiza ambaye anatumia nguvu nyingi kulima bila kupata faida.

 "WRRB tupo tayari na milango  ipo wazi ili tuweze kukaa pamoja  kujadiliana ni namna gani na wao watawaingia katika Mfumo ili waendelee kunufaika badala ya kuuangalia mfumo kama changamoto,"amesema.

Bangu ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa Mfumo 2007, 2008 hadi 2020/2021 ukuaji wa uzalishaji umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa asilimia 12, kwa mwaka ikilinganishwa na ukuaji wa  asilimia 2 wa mwaka kabla ya kuanzishwa kwa mfumo huo  huku akitolea mfano katika zao la Korosho mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo palikuwa na ongezeko la asilimia 164 la bei kutoka Ths 350.00 msimu wa 2006 hadi 2007.

Akizungumzia mafanikio yaliyopatikana baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi za ghalani amesema kuwa ni pamoja na ongezeko la bei za mazao, mapato ya mkulima na mapato ya Serikali kwa wastani wa asilimia 200 kutokana na urasimishaji, ongezeko la uzalishaji wa mazao kwa wastani wa asilimia 12 kwa mwaka na kichecheo cha ubora wa mazao yanayofikishwa sokoni.

Mkurugenzi huyo ametaja mafanikio mengine ni upatikanaji wa takwimu sahihi za mazao yanayopita kwenye mfumo wa stakabadhi za ghala, ongezeko la mapato ya uhakika kwa Serikali kuu na Serikali za mitaa na kukuza huduma za fedha vijijini,kufanikisha uanzishaji wa Soko la bidhaa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI