NEEC LIMERATIBU MKOPO ZAIDI YA TRILIONI 5, WANAWAKE WASHAURIWA KUTOKUCHUKUA MIKOPO YA KAUSHA DAMU


Na Asha Mwakyonde,Dodoma

BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), limesema kuwa limewafikia watanzania milioni 9.8 katika kipindi cha mwaka 2022 kwa kuwapatia mkopo wa shilingi trilioni 5.6.

Pia limewashauri  wananchi kuacha kukopa mikopo umiza kiholela  (KAUSHADAMU) na baadala yake wameshauriwa kuchukua fedha hizo kwa Matumizi lengwa kutokana na  wanawake wengi kuchukua mikopo na kufanya mambo yasifaa ambapo baadae inawasababishia kushindwa kurejesha mkopo huo kwa wakatu.

Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo Februari 14, 2023 na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo NEEC Beng'i Issa alipokua akielezea utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo amesema kutokana na hali hiyo Baraza limetoa elimu kwa wananchi kupatiwa elimu ya Fedha ili wasijikute wameingia katika mikopo hiyo umiza (KAUSHADAMU).

Beng'i amesema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi hasa wakina mama wanaochukua mikopo kwa lengo la kufanyabiashara na  badala yake wanatumia mikopo hiyo kufanya shughuli nyingne ambazo sio za kiuchumi na kusababisha mgogoro wakati wa marejesho.

Amefafanua  kuwa wapo wananchi wanaochukua mikopo na kulipa ada mashuleni hata kufanyia shughuli za ujenzi wa nyumba bila kujua atarejesha vipi mkopo aliochukua na baadae kusababisha migogoro katika kurejesha.

"Wanawake wanafikiri kujikwamua kiuchumi ni kwenda kuchukua pesa lakini katika uwezeshwaji tunataka pesa iwe kitu cha mwisho, Tumekubaliana na Wizara ya Elimu  tutoe elimu ya fedha na tuingize kwenye mitaala kwa kuwa tatizo tulilonalo Watanzania hatusomi kabisa elimu ya Fedha.”ameeleza.

Baraza lina majukumu ya kuwezesha kubuni, kupanga, kusimamia, kufuatilia, kutathmini na kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wa kiuchumi nchini
na linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali ambazo ni Ardhi, Mitaji,Ushirika, Ubinafsishaji Masoko na Ujuzi.

NEEC ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa na Sheria ya 16 ya 2004 kama njia ya kuharakisha mchakato wa kuwawezesha Watanzania kiuchumi.

Bi Beng'i amesema NEEC ndio chombo pekee kinachosimamia Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local Content) hapa nchini
ambapo hadi sasa kuna kampuni zaidi ya 1,770 za Kitanzania zilizopata tenda katika miradi ya kimkakati na zaidi ya Watanzania 83,000 wamepata ajira katika miradi hiyo.

Baraza linasimamia na kuratibu mifuko na programu za uwezeshaji nchini na kuna mifuko zaidi ya 72 inayosimamiwa ikiwa ni pamoja na Mifuko inayotoa mikopo moja kwa moja, Mfano Women Development Fund, SELF Microfinance,Mifuko inayotoa dhamana, Mfano PASS Trust, Mfuko wa Nishati Jadidifu ,Mifuko inayotoa ruzuku, Mfano TASAF, Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF).

NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) hapa wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa.

Baraza hilo linatoa usimamizi wa vikundi vidogo vya fedha pamoja na kuvilea pia kuvipa ushauri wa ni jinsi gani viweze kuendelea, jukumu hili limeanza tangu mwaka 2010 hadi sasa

“NEEC hadi sasa imewezesha kuwapatia ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini Kadhalika NEEC inasimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika mikoa yote 26, na Halmashauri zote nchini," amesema

 Baraza huandaa Makongamano ya Kitaifa na Maonesho ya Mifuko na programu za Uwezeshaji ili kuongeza na kukuza uwezo kwa walengwa ambayo ni Kongamano la mwaka la Uwezeshaji, Kongamano la Ushiriki wa Wananchi katika Miradi ya Kimkakati, Maonesho ya mifuko na programu za Uwezeshaji.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI