TBA UNA UPUNGUFU WA WATUMISHI ZAIDI YA 400

 

Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA), unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi 461 ambapo waliopo ni watumishi 350 ili kutekeleza majukumu ya Wakala huo na kwamba umekuwa ukitoa ajira za mikataba.

Pia umeishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha Wakala huo kiasi cha shilingi bilioni 54.2 kwa kipindi cha miezi 18 ,lengo likiwa ni kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati  pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali.

Hayo yamesemwa jijini Dodoma Februari 14 na Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch Daud Kondoro wakati akizungumzia  utekelezaji wa majukumu ya wakala huo katika kipindi cha miaka miwili, ameeleza kwa mujibu wa muundo wao wanatakiwa kuwa na watumishi 811.

Arch Kondoro amefafanua kuwa ili kujazia idadi hiyo wamekuwa wakitoa ajira za muda kwa mikataba kukingana na  shughuli za mradi wanayotekeleza kupitia wakala huo.

"Naishikuru Serikali kwa kuweza kutupatia kibali cha kuajiri ili kutekeleza majukumu yetu kupitia miradi mbalimbali ikiwamo ya kimkakati," amesema Mtendaji huyo.

Amesema kuwa changamoto nyingine ni ukosefu  wa vifaa kutokana na majukumu ya ya ujenzi inawalazimu kununua kokoto kulingana na bei  iliyopo sokoni kwa wakati wanapohitaji.

Mtendaji huyo amesema kuwa moja kati ya maelekezo ambayo wameyapata kutoka kwa viongozi wao kuona ni namna gani wanaweza kupata eneo la mgodi kwa ajili ya kokoto ili waweze kutekeleza majukumu yao.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI