SERIKALI IPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA WADAU WA HABARI


Na Asha Mwakyonde,Dodoma 

Naibu Waziri wizara ya habari mawasliano na Taknologia ya habari Mhandisi Kundo Methew amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote wa sekta ya habari na utangazaji katika maendeleo ya Taifa.

Mhandisi Methew amesema hayo leo Februari 13,2023 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji Tanzania uliyoenda sambamba na siku ya radio Duniani.

Amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na wadau wa habari na utangazaji, huduma ya utangazaji imekuwa na mabadiliko makubwa huku vyanzo vya mapato vya kuendesha vituo vikiwa vilevile,na huduma ya utangazaji Kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo ya biashara na ufadhili wa vipindi kutoka kwa wafadhili.

Aidha Tekinologia ya Internet nayo imebadilisha huduma za utangazaji Duniani,watu wengi wamehamia kwenye jukwaa la Internet kupata habari na huduma nyingine kwa njia ya kielectronic.

Kuhusu Changamoto za kiuchumi kwenye vyombo vya utangazaji Mhandisi Methew amesema kuwa Serikali imechukua hatua ya kupunguza ada za mwaka za leseni za utangazaji kwa takribani asilimia 40 pia imeweza kupunguza ada za masafa Kwa maeneo ambayo hayana tija kibiashara na imeunda kamati ya kuchunguza uchumi wa vyombo vya habari ili kupata hali halisi ya changamoto wanazopitia.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI