Dk. BITEKO AMTAKA KATIBU MKUU MPYA KUWAONA WATUMISHI WA SEKTA YA MADINI NI WATU MUHIMU

 Na Asha Mwakyonde, Dodoma

WAZIRI wa Madini Dk.Doto Biteko amemtaka Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Kheri Mahimbali kuhakikisha na kuwaona watumishi ni watu muhimu kwa kuwa wanatumia muda wa saa nane kazini tofauti na muda wanaotumia wakiwa wakiwa nyumbani.

Pia Waziri Dk Biteko amempongeza na kumshukuru  Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaongezea timu ya wachapakazi katika Wizara hiyo.

Waziri Dk. Biteko ameyasema hayo jijini Dodoma Machi 10,2023 katika kikao cha kumtambulisha Katibu huyo kwa watumishi  wa Idara zote zilizopo sekta ya madini  ameeleza lengo ni kusimamia malengo waliyowekwa na serikali.

Amesema watumishi hao muda mwingi wanautumia wakiwa kazini na kwamba nyumbani wanatumia saa tatu huku wakisinzia hivyo wanapaswa kuonwa wao ni watu muhimu katika Wizara hiyo.

"Wafanyakazi hawa hakikisha wanajiona wao ni watu muhimu na wapo wa kila aina na tabia zote unazozifahamu hapa duniani hivyo unapaswa kuwaelewa vizuri. Tuna malengo ambayo tumepewa na nchi tuyasekume yaende salama,"amesema Dk. Biteko.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hivyo  Msafiri  Mbibo amesema kuwa  sekta ya madini ni muhimu katika uchumi, maisha na maendeleo kiujumla na kwamba rasilimali za madini zilihifadhiwa na waasisi wa nchi hivyo wataendelea kuzisimamia kwa maslahi ya Watanzania.

"Tumepewa dhamana ya kuzisimamia na kufanya utekelezaji mzuri na wenye tija kwa maslahi mapana na nchi yetu, tuna vitu vitatu ambavyo tunatakiwa kuviangalia kama Wizara vikiwamo uadilifu ,uwahibikaji na njonzi pana ambazo ni za kuzisimamia rasilimali za madini," amesema.


Post a Comment

0 Comments

CHATANDA:RAIS DK. SAMIA AMEIMARISHA SEKTA YA MADINI